Tuesday, August 13, 2013

Jeshi la Polisi Dar latangaza dau la Sh100 milioni kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa za kundi la uhalifu linalojihusisha na vitendo vya kuwamwagia maji baadhi ya watu yanayodhaniwa ni tindikali


 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova
--
 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetangaza kutoa donge nono la Shilingi milioni 100/= kwa mtu yeyote atakayewezesha kupatikana kwa taarifa za kundi la uhalifu linalojihusisha na vitendo vya kuwamwagia na kuwadhuru watu tindikali.
 
Hatua hiyo inatokana na vitendo hivyo kushamiri maeneo mbalimbali nchini.Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema vitendo hivyo havipaswi kuvumiliwa na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwafichua watu hao.
 
“Nimeamua kuomba fedha hizi serikalini ili nimpe mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa hizo, hatimaye kukomesha vitendo hivi. Kemikali hii imekuwa na madhara makubwa,” alisema Kova.
 
Hivi karibuni Mkurungezi wa Maduka ya Home Shopping Center, Mfanyabiashara wa Lebonon na raia wawili wa Uingereza walimwagiwa maji yanayodhaniwa ni tindikali.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...