Mwanamuziki Diamond Platnum akimkabidhi funguo ya gari aina ya
Toyota Funcargo mwanamuziki mkongwe nchini mzee Muhidin Gurumo
kama zawadi yake kwa mkongwe huyo wa muziki baada ya kustaafu rasmi
kuimba muziki, Diamond alitoa zawadi hiyo kwa Gurumo katika hafla
yake ya uzinduzi wa video yake mpya ya wimbo Nomber One aliyoirekodi
huko Afrika Kusini ikigharimu kiasi cha dola elfu 30.000 zaidi ya milioni
arobaini za Tanzania, Video hiyo imetengenezwa kwa viwango vya kimataifa
na itaweza kumtangaza vyema kijana huyo wa kitanzania katika ulimwengu
wa muziki hasa kimataifa, Hafla hiyo imefanyika kwenye hoteli ya Serena
Dar es salaam na imehudhuriwa na wasanii pamoja na waigizaji wa filamu
na watu maarufu mbalimbali
Mzee Muhidin Gurumo akimshukuru Diamond kwa kumzawadia gari jambo ambalo kwake ni kama ndoto kwakuwa amestaafu akiwa hana usafiri “Yaani sijui hata mke wangu nikimwambia atanielewaje manake ni jambo la kushangaza kwangu” Alisema mzee Gurumo
Diamond akimuongoza mzee Gurumo kwenda kumuonyesha gari
Diamond akimuonyesha Mzee Gurumo gari
Akimuelekeza jambo baada ya mzee Gurumo kuingia kwenye gari
Mzee Gurumo akihojiwa na waandishi wa habari
Kulia ni Irene Uwoya kushoto Salma Msangi
Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akiwa na mama yake Diamond
Kutoka kulia ni Raymond Kigosi, Irene Uwoya na JB wakiwa katika hafla hiyo.
Wadau mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo. Picha zote na John Bukuku
No comments:
Post a Comment