.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini
(UNIC) Stella Vuzo akielezea jukumu lao kubwa wao kama Unic ni
kuelimisha jamii ambapo kwa kufanya hivyo wamehamasika kuanzisha
vilabu vya kujisomea kwa shule za msingi vitakavyowajengea watoto
msingi mzuri wa kupenda kujisomea ili kufahamu mambo mengi zaidi
yanayoendelea duniani katika nyanja ya Sayansi, Teknolojia na habari.
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha ( wa tatu kushoto)
na Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika
kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni
Mama Demere Kitunga ( wa nne kushoto) wakikabidhi vitabu vya
kujisomea kwa walimu na baadhi ya wanafunzi wa shule ya
msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC)
Stella Vuzo akishiriki zoezi hilo la kukabidhi vitabu kwa baadhi ya wanafunzi
wa shule ya Msingi Oysterbay wakihamasisha wanafunzi kujenga tabia ya
kujisomea tangu wakiwa wadogo.
Afisa Habari wa UNIC Usia Nkhoma Ledama naye alishiriki zoezi hilo.
Mwalimu Salome Makanza (kushoto) akitoa shukrani kwa kituo cha
habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) kwa msaada huo ambapo
waliahidi kuleta mabadiliko ya maendeleo kwa wanafunzi wao kujijengea
tabia ya kujisomea na hata kuongeza ufaulu kwa matokeo ya darasa la
saba shuleni hapo. Katikati ni Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet
Macha na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki
katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni
Mama Demere Kitunga.
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha akitoa ushauri wa
namna ya upangaji vitabu kwa Msimamizi wa Maktaba ya shule
hiyo Mwl. Veronica Kassidy.
Unic team wakijikumbushia baadhi ya vitabu walivyowahi kuvisoma
walipokuwa shule za msingi.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay wakichagulia
vitabu vya kujisomea katika maktaba ya shule yao.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika
kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni
Mama Demere Kitunga na Afisa Habari wa UNIC Stella Vuzo
wakiteta jambo na baadhi ya wanafunzi wa shule mara baada
ya kumaliza zoezi la kukabidhi vitabu wanafunzi hao.
No comments:
Post a Comment