Meneja Uhusiano wa
Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akizungumzia kampeni ya Pamoja
na Vodacom namna inavyotekelezwa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa
Ramadhani kwa kuandaa futari na kutoa sadaka ya vyakula na vifaa vya shule kwa
wanafunzi wa madrasa sehemu mbalimbali nchini. Mwaka huu Vodacom Foundation
ilitenga Sh. 50 Milioni kwa ajili ya kampeni hiyo na kuwafikia wanafunzi zaidi
ya 2500.
Mfanyakazi wa Vodacom
Tanzania Jaffary Juma akikabidhi vyakula vilivyotolewa na Vodacom Foundation
kwa wanafunzi wa madrasa mbalimbali za Kisiwani Pemba tukio lililohusisha pia
futari kwa ajili ya wanafunzi hao na wadau wa Vodacom Kisiwani humo
iliyofanyika uwanja wa Gombani mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni Kadhi Mkuu
wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis(mwenye koti jeusi) na Mwenyekiti wa
Vodacom Foundation Hassan Saleh (kulia) na wafanyakazi wa Vodacom.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Khamis Haji Khamis(mwenye koti jeusi) na Mwenyekiti wa Vodacom
Foundation Hassan Saleh (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
Vodacom na baadhi ya wanafunzi wa Madrasa za Kisiwani Pemba mara baada ya zoezi
la kukabidhi sadaka ya vyakula na vifaa vya shule kwa wanafunzi hao muda mfupi
kabla ya wote kushiriki futrari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwenye
uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba mwishoni mwa wiki
Kadhi Mkuu wa
Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis akisalimiana na viongozi mbalimbali wa dini
ya kiislamu wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Uwanja wa Gombani Pemba tayari
kuongoza hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na Vodacom Foundation mwishoni mwa
wiki kwa ajili ya wanafunzi wa Madrasa na wadau wa kampuni hiyo. Kulia ni
Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh
No comments:
Post a Comment