Friday, August 30, 2013

TAARIFA RASMI YA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) KUHUSU TUKIO LA KUFARIKI KWA AFISA WA JWTZ KATIKA JUKUMU LA KULINDA AMANI-DRC,GOMA

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
Simu ya Upepo  : “N G O M E”                                             Makao Makuu ya Jeshi,

Simu ya Mdomo  : DSM  22150463                                         Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                                       DAR ES SALAAM,   29  Agosti, 2013.
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe         : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                   : www.tpdf.mil.tz
                
--
1.       Kama mnavyofahamu, JWTZ linashiriki katika operesheni za Umoja wa Mataifa huko Goma DRC. Kikosi chetu kimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani kama kinavyopangiwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini DRC lijulikanalo kama MONUSCO

2.       Tarehe 28 Agosti 2013 Wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la Ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha Majeruhi. 

Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu, na hali zao zinaendelea vizuri.
3.       MONUSCO inaandaa utaratibu wa kuleta mwili wa Marehemu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.  
Dar es Salaam.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...