Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya kusaka mshindi wa nyumba wa kwanza kupitia Promosheni ya Airtel Yatosha. Kushoto ni Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bw. Mrisho Milao, kulia ni Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga wa kwanza kulia. Droo ya Airtel Yatosha ilimpata mshindi wa Nyumba Bw Silvanus Juma kutoka mkoa wa Iringa.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando, Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bw. Mrisho Milao (kushoto) na Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga wa kwanza kulia wakisubiri draw ya kutafuta mshindi itafute namba ya mshindi wakati wa kutafuta mshindi wakati wa kuchezesha droo ya kusaka mshindi wa nyumba wa kwanza kupitia Promosheni ya Airtel Yatosha. Droo ya Airtel Yatosha ilimpata mshindi wa Nyumba Bw Silvanus Juma kutoka mkoa wa Iringa.
Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga wa kwanza kulia akizungumza na simu ya mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel wakati wa kutafuta mshindi wakati wa kuchezesha droo ya kusaka mshindi wa nyumba wa kwanza kupitia Promosheni ya Airtel Yatosha katikati ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando na Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bw. Mrisho Milao (kushoto) . Droo ya Airtel Yatosha ilimpata mshindi wa Nyumba Bw Silvanus Juma kutoka mkoa wa Iringa.
**************************************88
Airtel
Tanzania imetangaza mshindi wa kwanza wa nyumba kupitia promosheni ya
Airtel Yatosha Shinda nyumba inayoendelea na kuwazawadia wateja wake
kila siku Bwana Silvanus Juma mkazi wa Iringa mwenye umri wa miaka 33
ambaye ni mhasibu katika shirila la Tanzania Rural women and children
development foundation - TARWOC ameibuka mshindi na kuzawadiwa nyumba
kisasa iliyojengwa na shirika na nyumba la taifa NHC iliyopo kigamboni
jijini Dar es Saalam.
Akiongea wakati wa kuchezesha droo hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel
bwana Jackson Mmbando alisema" kama tulivyowangazia awali leo ndio ile
siku muhimu na maalumu ya kumpata mshindi wetu wa kwanza wa nyumba na
tumeshuhudia bwana Silvanus Juma akiibuka mshindi kupitia droo ya
kwanza tuliyoichezesha hapa.
Sambaba na hilo leo tunao washindi 7 wa wiki kutoka katika mikoa
mbalimbali ambao hawa wataondoka na pesa taslimu shilingi milioni moja
kila moja, washindi hawa ni pamoja na Peter Ignasho kutoka Muheza
Tanga, Edita Rweyabura kutoka Bukoba, Steven Maguro , Rakesh Ali Mauji,
Mwajuma Hassani kutoka Dar es Saalam, Siasa Yahaya Songo kutoka Manyoni
Singida and Vero Mispela Kiwango kutoka Bihalamulo.
Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kuendelea kutumia huduma ya
Airtel yatosha na kujiunga na vifurushi mbalimbali na kupata nafasi ya
kujishindia zawadi mbalimbali , kujiunga nirahisi piga *149*99# kisha
nunua kifurushi chacko cha siku, wiki au mwezi na kisha kuingizwa moja
kwamoja kweny droo ya kuweza kushinda milioni moja kila siku au zawadi
kubwa ya Nyumba.
Akiongea mara baada ya kutangazwa mshindi Bwan Silvanus Juma
alisema"Ninayofuraha sana kupata zawadi hii kubwa kutoka Airtel napenda
kutoa wito kwa watanzania na wateja wa Airtel waendelee kutumia huduma
ya Airtel yatosha na waamini kuwa hakuna upendeleo.
Binafsi sijawahi kushinda Bahati nasibu yoyote na nilikuwa siamini
kama hakuna ubaguzi kwenye kushinda, lakini leo nashuhudia kwamba
ushindi ni wa uhakika usio na upendeleo wala ubaguzi hivyo wajaribu nao
wanaweza kuwa washindi.
Kwa upande wake moja ya wafanyakazi wenzake Bwana Beatus Magoti
ambaye ni Mshauri wa fedha na utawala TARWOC alisema" tumefurahi sana
kuona kijana mgodo mwenzetu ambaye ni mchapa kazi ameweza kushinda
nyumba kupitia promosheni ya Airtel yatosha. Hii imetupa hamasa na sisi
kushiriki na kueneza habari kwa wengine kushiriki na kushinda kama
laivyoshinda Silvano.
Airtel inaendelea na promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba tatu
ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake na kutoa huduma bora zenye
gharama nafuu kupitia huduma ya Airtel yatosha. Sambamba na hilo Airtel
pia imewawezesha wateja wake nchi nzima kutuma na kutoa pesa bure bila
makato yoyote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment