Friday, August 30, 2013

AIRTEL YATOSHA ; NYUMBA YA PILI ZIMEBAKI SIKU 5 TU!!!‏

Nyumba ya kisasa ya Airtel Yatosha inayoshindaniwa.

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akiongea na wanahabari.…

Nyumba ya kisasa ya Airtel Yatosha inayoshindaniwa.

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akiongea na wanahabari.

...Akionyesha funguo za nyumba inayoshindaniwa.

· DROO KUCHEZWA TAREHE 5/09/2013 AIRTEL MAKAO 
MAKUU DSM
Airtel Yatosha inazidi kupamba moto. Zimebaki siku CHACHE SANA
 kwa wewe MTEJA wa Airtel kuibuka mshindi wa Nyumba ya kisasa 
ya Airtel Yatosha iliyojengwa na Shirika la nyumba la taifa (NHC) iliyopo 
maeneo ya kigamboni jijini Dar es saalam.

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando amesema “Siku ya 
Alhamisi tarehe 5 mwezi wa 9 ndio siku inayosubiriwa kwa hamu; 
ambapo tutapata mshindi wa nyumba ya pili ya promosheni ya Airtel 
Yatosha”
Wewe mteja wa Airtel Yatosha bado una nafasi ya kuibuka mshindi! Ni 
rahisi. Piga *149*99# sasa na ujiunge na kifurushi chochote cha SIKU, 
WIKI AU MWEZI cha Airtel Yatosha na moja kwa moja utaingia kwenye
 droo ya kushinda. Kumbuka, pia kuna Tsh milioni 1 kushindaniwa kila siku. 
Usilaze damu! Jiunge zaidi na Airtel Yatosha, uongeze nafasi zako za kushinda! 
Alidokeza bw, Mmbando.

NBC yazindua Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza
 katika hafla ya uzinduzi waKitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki 
kwa Wateja Wakubwa cha NBC jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kushoto)
 akiwatambulisha baadhi ya maofisa katika kitengo hicho katika hafla hiyo.

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akifurahi 
na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu (kushoto) na Mkuu wa Idara
 ya Huduma za Kibenki kwa Wateja Wakubwa na Uwekezaji, Andre Potgieter
 katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa 
Wateja Wakubwacha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akishikana
 mikono na Meneja Uhusiano wa NBC, Makyalen Marealle katika hafla ya uzinduzi 
wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki 
hiyo jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo
 hicho, Andrew Massawe na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akihojiwa
 na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya uzinduzi wa
 kitengo hicho. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kulia) akimsindikiza 
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi mara baada ya uzinduzi wa Kitengo 
cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini
 Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Huduma Rejareja 
za Kibenki wa NBC, Mmoloki Legodu na Mkuu wa Kitengo hicho, Andrew Massawe.

RAISI JAKAYA MRISHO KIKWETE ATEUA MKUU MPYA WA UHAMIAJI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule kuwa Kamishna Mkuu, Idara ya Uhamiaji.
 
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Agosti 28, mwaka huu, 2013.
Ndugu Mwakinyule anachukua nafasi ya Ndugu Magnus Ulungi ambaye atapangiwa kazi nyingine.
 
Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule, alikuwa Naibu Kamishna wa Uhamiaji na Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania, London, Uingereza
 
Rais pia amemteua Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda.
 
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana Agosti 28, mwaka huu, 2013.
 
Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro alikuwa Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji (Productive Sectors) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

MWANAMUZIKI DIAMOND AMKABIDHI GARI MWANAMUZIKI MKONGWE(MSTAAFU)MZEE MUHIDIN GURUMO,KATIKA HAFLA YA UZINDUZI WA VIDEO YAKE


 Mwanamuziki Diamond Platnum akimkabidhi funguo ya gari aina ya 
Toyota Funcargo mwanamuziki mkongwe nchini mzee Muhidin Gurumo 
kama zawadi yake kwa mkongwe huyo wa muziki baada ya kustaafu rasmi 
kuimba muziki, Diamond alitoa zawadi hiyo kwa Gurumo katika hafla 
yake ya uzinduzi wa video yake mpya ya wimbo Nomber One aliyoirekodi
 huko Afrika Kusini ikigharimu kiasi cha dola elfu 30.000 zaidi ya milioni 
arobaini za Tanzania, Video hiyo imetengenezwa kwa viwango vya kimataifa 
na itaweza kumtangaza vyema kijana huyo wa kitanzania katika ulimwengu 
wa muziki hasa kimataifa, Hafla hiyo imefanyika kwenye hoteli ya Serena 
Dar es salaam na imehudhuriwa na wasanii pamoja na waigizaji wa filamu
 na watu maarufu mbalimbali
 Mzee  Muhidin Gurumo akimshukuru Diamond kwa kumzawadia gari jambo ambalo kwake ni kama ndoto kwakuwa amestaafu akiwa hana usafiri “Yaani sijui hata mke wangu nikimwambia atanielewaje manake ni jambo la kushangaza kwangu” Alisema mzee Gurumo
 Diamond akimuongoza mzee Gurumo kwenda kumuonyesha gari
 Diamond akimuonyesha Mzee Gurumo gari
Akimuelekeza jambo baada ya mzee Gurumo kuingia kwenye gari
 Mzee Gurumo akihojiwa na waandishi wa habari
 Kulia ni Irene Uwoya kushoto Salma Msangi
 Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akiwa na mama yake Diamond
 Kutoka kulia ni Raymond Kigosi, Irene Uwoya na JB wakiwa katika hafla hiyo.
 Wadau mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo. Picha zote na John Bukuku

TAARIFA RASMI YA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) KUHUSU TUKIO LA KUFARIKI KWA AFISA WA JWTZ KATIKA JUKUMU LA KULINDA AMANI-DRC,GOMA

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
Simu ya Upepo  : “N G O M E”                                             Makao Makuu ya Jeshi,

Simu ya Mdomo  : DSM  22150463                                         Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                                       DAR ES SALAAM,   29  Agosti, 2013.
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe         : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                   : www.tpdf.mil.tz
                
--
1.       Kama mnavyofahamu, JWTZ linashiriki katika operesheni za Umoja wa Mataifa huko Goma DRC. Kikosi chetu kimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani kama kinavyopangiwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini DRC lijulikanalo kama MONUSCO

2.       Tarehe 28 Agosti 2013 Wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la Ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha Majeruhi. 

Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu, na hali zao zinaendelea vizuri.
3.       MONUSCO inaandaa utaratibu wa kuleta mwili wa Marehemu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.  
Dar es Salaam.

Jopo la Madaktari Bingwa Saba wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wafanikiwa kuwatenganisha pacha waliokuwa wameungana kiwiliwili

Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Muhimbili, Profesa Karim Manji (wa pili kushoto) akifurahia na wenzake baada ya kufanikiwa kwa operesheni ya kuwatenganisha watoto walioungana, kazi iliyofanywa na jopo la madaktari bingwa saba kwa saa 4. Picha na Michael Jamson
---
  Jopo la Madaktari Bingwa Saba wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa ya hospitali hiyo (Moi), wamefanikiwa kuwatenganisha pacha waliokuwa wameungana kiwiliwili.
 
Iliwalazimu mabingwa hao kutumia saa nne kufanikisha upasuaji huo. Mmoja wa watoto hao waliotenganishwa, amelazwa kwenye Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU) Taasisi ya Mifupa Moi wakati kiwiliwili kingine kilifariki.
Jopo la madaktari waliofanikisha upasuaji huo ni; bingwa mstaafu wa watoto ambaye aliitwa maalumu kwa kazi hiyo, Petronila Ngiloi, Dk Robert Mhina (mifupa) na Profesa Karim Manji aliyekuwa akifuatilia kwa karibu mapigo ya moyo.
Wengine ni Dk Karima Khalid aliyekuwa akiratibu dawa ya usingizi, Dk Hamis Shaaban (ubongo na uti wa mgongo), Dk Zaitun Bokhary (bingwa upasuaji watoto) na Dk Nyangasa (moyo na mishipa ya fahamu).Kwa habari zaidi bofya na Endelea......>>>>>

Thursday, August 29, 2013

Wadau walivyomuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13, akabidhiwa Bendera ya Taifa


Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred
  Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akikumbatiana na Mama yake Mzazi wakati wa Kumuaga.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akimuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (katikati) mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara  (kulia) wakati wa hafla ya Chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Mrembo huyo,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe,Jijini Dar es Salaam usiku huu.
  Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akimkabidhi Bendera ya Taifa,Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013).Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko (pili kulia),Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kulia) pamoja na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
  Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akitoa shukrani zake wakati wa hafla hiyo ya kumuaga iliyofanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akitoa nasaha zake kwa Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2013,wakati wa hafla ya Chakula cha jioni ikiwa ni sehemu ya kumuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World).Hafla hiyo imefanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko na kushoto ni Mlezi na shoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akizungumza machache ikiwa ni pamoja na kuwaasa Warembo waliopo kambini hivi sasa kujitahidi kufanya vyema.
  Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Giraffe,Dkt. Charles Bekoni akitoa salamu.
  Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko akiongea machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza.
Sehemu ya Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa kwenye hafla hiyo.Picha zote na Othman Michuzi

EDWARD LOWASSA ASHEHEREKEA MIAKA YAKE 60 YA KUZALIWA


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli mkoani Arusha, Edward Lowassa akilishwa kipande cha keki na mkewe wakati wa maadhimisho ya siku yake ya Kuzaliwa ambapo kiongozi huyo alitimiza miaka 60 Agosti 26, mwaka huu. Tafrija hiyo ambayo alijumuika na wajukuu zake ilifanyika nyumbani kwake Monduli.
 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli mkoani Arusha, Edward Lowassa akimlisha keki mkewe wakati wa maadhimisho ya siku yake ya Kuzaliwa ambapo kiongozi huyo alitimiza miaka 60 Agosti 26, mwaka huu. Tafrija hiyo ambayo alijumuika na wajukuu zake ilifanyika nyumbani kwake Monduli.  
 waziri mkuu mstaafu na mbunge wa monduli Mh Edward Lowassa akiwa na wajukuu zake tayari kukata keki ya sherehe ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake tarehe 26 aliyoandaliwa na mkewe mama Regina Lowassa huko Hekima Garden mikocheni.

 Wajukuu wakimwimbia Babu Happy Birthday!!
 Mishumaa iliwashwa

 babu kata kekiii tuleeeeeee 
 Bibi alisaidia kukata keki hiyo...
 Makamanda wakiisubiri kwa hamu....
 kumbato la pongezi kutoika kwa mkewe.

 Mzee Lowassa akilishwa keki na mtoto wake Freddy Lowassa.
 Freddy nae akilishwa keki na baba.
SOURCE. http://mrokim.blogspot.com/

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...