Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela
----
Kwa siku za karibuni viongozi mbalimbali wa kitaifa na wastaafu wamekuwa wakitoa matamko ya kusisitiza amani nchini.
Dodoma/Pwani.Wakati Waziri Mkuu
Mstaafu, John Malecela ameonya Watanzania kuhusu mpasuko wa kidini
akibainisha kuwa utaigawa nchi vipande vipande, Rais Mstaafu, Ali Hassan
Mwinyi ametoa wito maalumu akiwataka waumini wa dini tofauti
kuvumiliana.
Malecela na Mwinyi walitoa kauli hizo mjini Dodoma
na Kibaha, Pwani jana kwa nyakati tofauti, wote wakiwa na nia ya
kusisitiza ulinzi wa amani ya nchi inayoanza kutetereka.
Kauli ya Malecela
Malecela alisema kwa namna ilivyo sasa, Tanzania
imekuwa ni tofauti na ile aliyoanza kuiona yeye katika kipindi cha uhuru
kwenye miaka ya 1960 wakati huo nchi ikiwa moja na watu wake wakiwa ni
wamoja.
“Msipokuwa makini na amani yenu, nchi hii mtaigawa
vipande vipande na kamwe amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa mambo ya
kusingiziana, badala yake tusaidiane sisi kwa sisi, na sisi na
viongozi,” alisema.Kwa Habari zaidi Bofya hapa na Endelea.......>>>>>>
No comments:
Post a Comment