Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa Arumeru
Magharibi, Goodluck Ole Medeye (katikati mwenye suti nyeusi) akipokea
sehemu ya msaada wa mifuko 200 kutoka kwa Meneja Mahusiano Jamii wa
Twiga Cement, Natasha D’Souza, iliyotolewa na kampuni hiyo kusaidia
waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha
Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru mkoani Arusha hivi karibuni.
Hafla ya makabidhiano ilifanyika Arusha mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa
Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (katikati mwenye suti nyeusi)
akimshukuru Meneja Meneja Mahusiano Jamii wa Twiga Cement, Natasha
D’Souza, baada ya kupokea msaada wa mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na
kampuni hiyo kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua
katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru mkoani
Arusha hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa
Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (kulia) akizungumza baada ya
kupokea msaada wa mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na kampuni ya Twiga
Cement kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika
kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi
karibuni. Kulia kwake ni Meneja Meneja Mahusiano Jamii wa Twiga
Cement, Natasha D’Souza.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa
Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (aliyeshika kamba kulia)
akisaidia maandalizi ya ujenzi wa daraja sehemu iliyoharibiwa na
mafuriko katika hafla ambayo kampuni ya Twiga Cement ilikabodhi msaada
wa saruji kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua
katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru mkoani
Arusha hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment