Mkuu
wa Wilaya ya Makete,Mh Josephine Matiro
akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake,mapema leo
mchana alipokuwa akikagua uhai wa mashina ya chama hicho katika kijiji
cha Tandala,Wilaya ya Makete mkoani Njombe.Kinana na
ujumbe wake wako ziarani mkoani Njombe katika kuimarisha shughuli za
chama,kuangalia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa CCM na pia
kuzungumza na
Wananchi kuhusiana na matatizo yao mbalimbali yanayowakabili .
Katibu
mkuu wa chama cha mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
Wananchi wa kata ya Iniho mapema leo jioni ndani ya wilaya ya Makete
mkoani Njombe,Kinana alizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara mambo
mbalimbali ikiwemo na kuwahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea
kutekekeleza miradi yake yote iliyoahidi ikiwemo ya barabara,maji na
umeme,aidha aliwataka wananchi kubeza baadhi ya vyama vya siasa
vinanvyoeneza chuki kwa watanzania na kuindosha amani iliyopo.Kinana
akiwa sambamba na ujumbe wake ameyazungumza hayo wilayani Makete katika
kijiji cha Ukwama ikiwa siku ya nne ya ziara yake mkoani Njombe
kutembelea mashina ya chama hicho pamoja na kufanya mikutano ya hadhara
kueleza serikali ilichotekeleza.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa Nape Nnauye akimtambulisha aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA, Keffa Lupiana pichani kushoto kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye kata ya Iniho,Wilaya ya Makete mkoani Njombe.
Mbunge
wa Jimbo la Makete na Naibu Waziri wa Maji Dkt.Binilith Mahenge
akieleza mambo mbalimbali ya kimaendeleo yaliyofanywa jimboni mwake
katika kutekeleza Ilani ya CCM kwenye mkutano wa .
Sehemu
ya Wananchi wakishangilia jambo wakati ndugu Kinana alipokuwa
akizunngumza nao kwenye mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa shule ya
msingi ya ukwama mapema leo jioni ndani ya wilaya ya Makete mkoani
Njombe .
Sehemu ya Wananchi wakiwa kwenye uwanja wa kata ya Ukwama wakimsubiri
Ndugu Kinana azungumze nao mapema leo jioni ndani ya wilaya ya Makete
mkoani Njombe.
Ndugu
Kinana akisalimiana akisalimiana Chifu wa kabila la Wakinga,Godfrey
Mwemusi Sanga,mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara uliofanyika leo
kwenye uwanja wa ukwama,wilaya ya Makete mkoani Njombe,shoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa Nape Nnauye
Sehemu ya hali ya hewa ya Wilaya ya Makete kama ionekavyo jioni ya leo. Picha na JIACHIE BLOG.
No comments:
Post a Comment