PROFESA JAY AJIUNGA NA CHADEMA TAYARI KWA KUENDELEZA MAPAMBANO YA KISIASA KAMA MKONGWE SUGU
Rapper mkongwe nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.
Profesa amekabidhiwa kadi ya uanachama wa CHADEMA na mbunge wa Mbeya
mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu.
Kujiunga rasmi kwa Profesa kwenye
chama hicho kunaashiria kuwa huenda akawa na nia ya kugombea ubunge kwa
tiketi ya chama hicho mwaka 2015.
Profesa ameamua kuweka wazi uamuzi wake baada ya watu wengi kuanza
kumuuliza maswali. “Mmeniuliza sana kwamba mimi ni CHAMA gani jibu
litapatikana Muda sio mrefu!! Still in Dodoma STAY TUNED,” alitweet.
No comments:
Post a Comment