Sunday, May 05, 2013

Bomu Lalipuka, mmoja afa kwenye uzinduzi wa Parokia mpya ya Olasiti, Jijini Arusha leo asubuhi mpaka sasa ni majeruhi 30

 Sehemu inayosadikiwa kitu kama bomu kulipuka
 Baadhi ya viatu vya waumini mbalimbali waliojeruhiwa
 Baadhi ya majerui wakiwa nje ya kanisa wakisubiri msaada wa kupelekwa hospitali.
 Picha Juu na chini ni baadhi ya majerui wakipatiwa matibabu hospitali
Picha juu ni baadhi ya wauminina viongozi mbalimbali wa kanisa wakiwa  nje ya kanisa muda mfupi baada ya kitu kichachosadikiwa kuwa ni bomu kulipuka nakusababisha majeruhi zaidi ya 30 leo asubuhi.Picha Zote kwa Hisani ya Mdau Frederick M. Katulanda
 ---
Na Mwandishi Wetu



MTU mmoja ambaye hajafahamika jina lake ameuwawa, mtoto mmoja hali yake ni mbaya na yu  mahututi na wengine zaidi ya 49 wakiwa wamejeruhiwa vibaya katika tukio la kulipuka bomu majira ya saa 5 leo asubuhi katika uzinduzi wa Parokia mpya ya Olasiti, Jijini Arusha wakati Askofu Mkuu Josephat Louis Lebulu na Balozi wa Baba Mtakatifu nchini, Askofu Mkuu  Francisco Montecillo Padilla wakiwa wamejiandaa kuanza maadhimisho ya misa ya kutabaruku kanisa hilo kwa kuwabariki waumini hao tayari kwa ibada.



Taarifa za awali zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas zinasema kuna majeruhi zaidi ya 30, lakini wanne walikuwa na majeraha makubwa, na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kuweza kuwabaini waliorusha na/au kutega bomu kwenye eneo hilo la Ibada.



Akiahirisha Ibada hiyo Vicar General wa Jimbo Katoliki la Arusha Padre Simon Tengesi aliwataka wakristo wote kuondoka eneo hilo na uzinduzi huo umeahirishwa hadi pale itakapotangazwa tena, na watu wameondoka eneo hilo ili kuruhusu vyomvyo vya ulinzi na usalama viweze kuanza uchunguzi.



Chanzo chetu cha habari kinasema eneo lilipolipuka bomu kuna damu nyingi na watu wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, Tutaendelea kuwajuza zaidi.

No comments: