Thursday, February 05, 2009
Republicans wamchagua mwenyekiti mweusi
Naibu Gavana wa Maryland, Michael Steele, amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Chama cha taifa cha Republicans (Republican National Committee). Ni mwuesi wa kwanza katika historia ya chama hicho kuongoza chama.
Kama mnakumbuka walivyofanya mkutano mkuu wao mwezi Agosti, weusi walikuwa wachache mno huko, uliweza kuwahesabu kwenye mkono. Na weusi wengine waliokuwepo walidai kuwa walitukanwa matusi ya kibaguzi. Kipindi hicho vyombo vya habari vilihoji uhaba wa weusi katika chama cha Repbulicans na kuuliza kama Republicans ni chama cha wazungu tu.
Huenda Republicans wanadhania kuwa wakiwa na Mwenyekiti mweusi basi labda weusi watavutiwa kujiunga na chama hicho.
Lazima kuna watu hapa ambao hawana raha kutokana na kuchaguliwa kwake. Wazungu walikuwa na usemi, "A Black Man will be President when Hell Freezes Over" yaani mtu mweusi atakuwa rais kipindi motoni kunageuka barafu tupu. Basi huo barafu umeingia motoni. Obama ni rais na Steele ni mwenyekiti wa Republicans.
Lazima wabaguzi wa KKK wanalia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment