Friday, February 13, 2009

JK amvua cheo DC aliyecharaza viboko walimu Bukoba

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Rais Jakaya Kikwete amemvua madaraka na kumwachisha kazi rasmi kuanzia jana mkuu wa wilaya ya Bukoba, Albert Mnali aliyeamuru polisi mmoja kuwachapa viboko walimu katika shule tatu za msingi zilizo wilayani kwake kutokana na kushika mkia katika matokeo ya darasa la saba.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Waziri Mkuu jana ilieleza kuwa Rais Kikwete amechukua hatua hiyo ili iwe fundisho kwa kuwa kitendo alichokifanya Mkuu huyo wa wilaya hakikubaliki, kimedhalilisha, cha kuvunja moyo walimu na kinavunja maadili ya kibinadamu.

Katika uamuzi huo, Rais Kikwete alisema mkuu huyo wa wilaya amedhalilisha wadhifa wa ukuu wa wilaya kwa kuwa alikosea kuchukua hatua hiyo kwa kuwa mwenye mamlaka ya kuwawajibisha walimu ni kamati za nidhamu za mikoa na wilaya na wala si mtu mmoja kama alivyofanya mkuu huyo.

Alisema kuwa amechukua hatua hiyo baada ya kufuatilia maelezo ya pande zote zinazohusika na kuwa serikali imeridhia kiongozi huyo avuliwe wadhifa.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...