Tuesday, February 10, 2009

Zombe ana kesi ya kujibu


WATATU WAACHIWA HURU
ZOMBEA ATOA SOMO LA SHERIA

HATIMAYE Mahakama Kuu imetegua kitendawili cha hatima ya aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoani Dar es Salaam, Abdallah Zombe na wenzake 12 baada ya kuamua kuwa wana kesi ya kujibu katika tuhuma zinazowakabili za mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva wa taksi mmoja, huku ikiwaachia watuhumiwa watatu.

Mahakama imeridhika kuwa washtakiwa hao watatu katika kesi hiyo namba 26 ya mwaka 2006 hawana kesi ya kujibu.

Zombe na wenzake wanashtakiwa kwa tuhuma za kufanya makosa manne ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka mjini Mahenge, Morogoro- Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi wa Manzese jijini Dar es salaam, Juma Ndugu.

Jaji wa Mahakama Kuu, Salum Masatti alisema mahakama hiyo imeridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kuwa Zombe, ambaye ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo na wenzake tisa wana kesi ya kujibu kuhusiana na vifo vya wafanyabiashara hao.

Washtakiwa wengine walioonekana wana kesi ya kujibu ni mshitakiwa wa pili ambaye ni Mrakibu wa Polisi (SP), Christopher Bageni, mshitakiwa wa tatu ambaye Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Ahmed Makelle na wa tano WP 4593 PC Jane Andrew.

Wengine ni mshitakiwa wa saba CPL Emmanuel Mabula, mshitakiwa namba tisa D.8289 PC Michael Sonza, mshitakiwa wa 10 D 2300CPL Ebeneth Saro, wa 11, D.9312D/C Rashid Lema, D4656 C/CPL Rajab Bakari na D.1367 D/CPL Festus Gwabisabi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...