Taarifa ambazo ambazo haziridhishi kabisa kuamini zimetufikia jana usiku kutokea Dodoma ambapo pia iliitishwa Press Conference usiku huo huo Slaa mwenyewe akidai kuwa aliwekewa vifaa vivyo vya kurekodi sauti. Mambo mawili ambayo naungana na ndugu yangu Maro inasikitisha kwamba tumeingia kwa mkumbo kwa mawazo ya kulia tu ni haya.
1.Kwanini tunashikilia Dk Slaa ndiyo amewekewa vifaa hivyo na watu ambao hawatuwafahamu ili khali inawezekana kabisa Dk Slaaa na CHADEMA wakawa wameweka vifaa hivi kama kujitafutia Umaarufu. Hilo Linawezekana na ni moja ya mbinu za kisiasa ili watu waendelee kuamini kuwa unaweza kuleta Mabadiliko. Tusubiri uchunguzi na iiwezekana Mzee Mwanakijiji na Bongo Radio any mahojiano na wale wahudumu wa ile Hotel.
2.Kuanza kuhisi kuwa ni Masha ndiyo kafanya jmbo hili,ama waziri kijana.Huu ni upotoishaji tena kwa hoja kwamba Masha alilipuliwa na Dr. Slaa. Kama tumefika katika siasa za chuki kama alivyosema Mzee Mkapa basi 2010 uchaguzi utakuwa ni wa aina ya ajbu kutokea katika Nchi hii.
2009/2/6 Josephat Isango
Watanzania ambao kwa muda huu mmelala fofofo, muda huu ni Saa saba Usiku, Dodoma hali sio nzuri usiku wa leo, Dr, wilbrod Slaa na Tarab Ally wamewekewa vitu vinavyosadikiwa kuwa ni vifaa vya kuwarekodi kwenye vyumba vyao vya kulala, kwenye sehemu za uvungu wa vitanda. hatujajua lengo la watu hao kuweka vifaa hivyo, ila ninachoweza kusema ni wabunge ambao wamekuwa na changamoto Bungeni, huenda kuna njama za Wabunge hao kuhujumiwa. Nchi yetu sijui inaenda wapi tuiombee.
5 comments:
Hatari lakini salama lakini huyu Masha anatatizo gani.sasa kila kona yeye anaguswa ilikuwaje namuomba bror ajiuzuru na kama wanamsingizia itakuwa afadhali kwake
chadema hawawezi siasa,walikuwa wanajinadi kwa sera ya ufisadi,sasa kikwete mewashuhulikia mafisadi,hawana cha kuwaambia wananchi,ndo maana wanatafuta sababu,lakini watu wameshawajua,ndo maana operation sangara imefeli dar kwa asilimia mia moja
we kazi yako kuripoti habari,mambo ya taarifa za uzushi wakati kla kitu kipo wazi sisi watanzania sasa tumeamka na tumechoshwa na ufisaDi,la utuambie HII BLOG NI YA CCM,na wewe ni mojawapo la fisadi,mbona unatetea tetea sana ndugu yangu?au we ni mojawapo au ndo wale waandishi wanakula kwa kuandikia wengine waneemeke?UNATUBOA SIO SIR!
Mwenyekiti,bwana Sewing Mchine, umeishiwa sasa!!!! Asilimia 65 ya waliogoma kupiga kura jimbo la Mbeya vijijini ni kina nani? Jibu-wanamsubiri mbunge wao mwakani-MTAJIJU!!! Kwa ufinyu wako na wenzio mafisadi,unafikiri waliofanya umafia ule chumbani kwa Dr. Slaa na yule wa CUF wangekuwa si CCM wangekuwa hawajapatikana hadi sasa?
Dr. Slaa aluta continua!!
serikali iliyo madarakani imeingia kwa asilimia zaidi ya 80,cuf wana asilimia 10,nyie chadema tano,sasa kelele za nini,watanzania wengi bado tunaiamini serikali yetu,chadema ni mafisadi wa roho,nafsi na mwili,msitake kuigeuza tz rwanda,watanzia wameamka,now ndo naamini kweli chama pekee cha upinzani tz kitabaki kuwa cuf,hawa wengine ni wakuja na kuondoka,maaana hawana sera,kazi majungu na kuchochea fujo,na kama hamtani kusoma ukweli humu,nendeni kwa mwanakijiji ukaongee udaku wenu,kule na mtanzania daima,maaana kule ndo watu akili zilizolala huchangia,mtu yeyote mwenye akili atajua dr slaa anatafuta umaarufu,hakuna chochote,usalama wa taifa hawawezi kutumia triki zakijinga kama hizo.lakini mwisho wa slaa 2010 na wapinzani kwa ujumla,karatu,moshi mjini na mpanda yanarudi ccm.na hapo ruzuku itakapopungua na waanzae kufanya kazi bills za kukata ticket
Post a Comment