Tuesday, February 10, 2009

Zombe amwaga chozi mahakamani

Ajitetea saa tatu

MSHTAKIWA wa kwanza katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka mjini Mahenge, Morogoro na dereva teksi wa Manzese jijini Dar es Salaam inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe jana alijikuta akimwaga machozi kizimbani wakati akiwasilisha utetezi wake.

Zombe alijikuta akimwaga machozi mara kadhaa wakati akijitetea mbele ya Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Salum Masatti kuhusiana na tuhuma hizo zinazomkabili yeye pamoja na askari wenzake tisa.

Hatua ya Zombe kupanda kizimbani jana na kuanza kujitetea ilikuja baada ya mahakama hiyo kuridhika kuwa yeye na wenzake wana kesi ya kujibu dhidi ya mauaji ya wafanyabiashara hao kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hoja za mawakili wa watuhumiwa hao na majibu ya hoja hizo kutoka kwa upande wa mashitaka. 

No comments:

RAIS SAMIA ALETA FURAHA NA MATUMAINI BUSEGA, AFUNGUA MRADI MKUBWA WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Shamrashamra za ufunguzi wa mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Lamadi, Wilayani Busega mkoani Simiyu tarehe 19 Juni, 2025 Rais wa Jamhur...