Thursday, February 12, 2009

DC acharaza walimu viboko

*Ni kwa matokeo mabaya darasa la saba
*Waziri asema katu hawawezi kuvumilia

MKUU wa wilaya ya Bukoba Albert Mnali, amemwamuru askari polisi mmoja kuwapiga viboko walimu katika shule tatu za msingi zilizoko Wilaya ya Bukoba kwa sababu wilaya hiyo imekua ya mwisho katika matokeo ya darasa la saba.

Tukio hilo lilitokea juzi wakati mkuu huyo wa wilaya Koplo wa polisi aliyeambatana naye kwa kuwalaza chini walimu hao na kumuamuru koplo huyo kuwadhibu viboko viwili makalioni na mikononi.

Walimu waliocharazwa viboko tisa wanatoka shule ya msingi Katerero, 11 wa shule ya msingi Kanazi ambao walichapwa viboko viwiwili kila mmoja na walimu 12 kutoka shule ya msingi Kansenene viboko vinne vinne kila mmoja.

Akizungumza jana waandishi wa habari juu ya tukio hilo mkuu huyo wa Wilaya alisema alilazimika kuwatandika viboko walimu hao baada ya kugunda au kuwepo uzembe kazini, ikiwemo kuchelewa kufika kazini na kutofundisha kama mikataba yao ya ajira inavyosema. Taarifa zaidi punde

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...