Wednesday, February 04, 2009

Nora bwana na mambo yake




KAMPUNI ya Beknet Tanzania Limited imeandaa uzinduzi wa albamu ya Upande wa Pili wa Ndoa isiyo ya Uaminifu katika Ukumbi wa Cinema wa Century Cinemax Mlimani City Februari 6.

Akizungumza na Mwananchi jijini jana, mkurugenzi wa filamu hiyo, Bariki Keenja alisema anatarajia uzinduzi wake utafana kwani katika filamu yake kuna mengi ya kufurahisha.

Alisema katika filamu hiyo, imezungumzia maisha halisi ambayo yapo katika jamii ya sasa ambapo mwanamke au mwanaume kumsaliti mwenzi wake kwa namna moja au nyingine na hii hutokana na tamaa zisizo na msingi.

Filamu hiyo imewashirikisha wasanii mbalimbali akiwemo Nuru Nasoro ''Nora'', Elizabeth Chijumba ''Nikita'', Ahmed Olotu anayetambulika kwa jina la kisanii, Mzee Chilo na Subira Maulid.

Pichani kulia Nora akisikiliza swali kwa makini kutoka kwa mmoja wa waandishi wa habari alipomuuliza kuhusiana na habari za kashfa ambazo zimekuwa zikimuandama muigizaji huyo juu ya mapenzi na wanaume tofauti tofauti

No comments:

Ziara za Viongozi na Taasisi za Umma Zapamba Moto Tarangire, TANAPA Yafaidi Ongezeko la Watalii wa Ndani

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linaendelea kunufaika na mwamko mkubwa wa watalii wa ndani, hususan kupitia safari za mafunzo...