Wednesday, February 25, 2009

Lipumba mwenyekiti tena



PROFESA Ibrahim Lipumba jana aliongoza viongozi wenzake wa Chama cha Wananchi (CUF) kuibuka na ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.

Lakini alikuwa ni katibu wake, Seif Sharif Hamad aliyeongoza kwa kura nyingi alipoibuka na ushindi wa asilimia 99.5, akiwa hana mpinzani katika kinyang'anyiro cha nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa Jaji Usi Haji Usi aliyetangaza matokeo hayo, Prof. Lipumba, ambaye alikuwa akichuana na Profesa Abdallah Safari na koplo Stephen Masanja, alishinda kirahisi nafasi ya uenyekiti alipozoa kura 646, ambazo ni asilimia 97 ya kura zote na kurudi kwenye nafasi yake atakayoishikilia kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Kura zote zilikuwa 665 upande wa Mwenyekiti tatu ziliharibika
646 Lipumba asilimia 97

Safari alipata kura asilimia 0.8

Masanja kura 10 ambazo ni asilimia 1.5

Kura zote za katibu mkuu 659
zilizoharibika 2
hapana 4

ndio 651 na ushindi ni asilimia 99.5

makamu kura zote 657

zilizoharibika 5

hapana 4

644 ambao ni ushindi wa asilimia 98.6

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...