Thursday, February 19, 2009

Msekwa mwenyekiti mpya TCD


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Pius Msekwa amesema, Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa Hassy Kitine ametumia haki yake ya kikatiba kutoa maoni kuhusu mwelekeo wa taifa.


Amesema yeye akiwa Kiongozi wa CCM hawezi kujadili maoni ya binafsi ya mtu kwani ni sawa na kuingilia haki yake.


Msekwa alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana alipotakiwa na Mwananchi kutoa maoni yake binafsi na CCM kufuatia kauli iliyotolewa na Kitine juzi kwamba tangu kipindi cha mwisho cha utawala wa Rais Benjamin Mkapa nchi, ilivurugika na kwamba maadili yameporomoka kuanzia ndani ya CCM.


Katika mkutano wake maalum na baadhi ya vyombo vya habari katika mgahawa wa Gymkana jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine Kitine alisema mfano wa kuoza kwa maadili ndani ya CCM upo wazi pale waziri anapojiuzulu wadhifa wake kwa tuhuma, lakini bado anabaki kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mbunge.


Akizungumza na Mwananchi jana katika hoteli ya Regency, Msasani, Msekwa alisema "Sioni kama ni utaratibu mzuri kutolea maoni yaliyotolewa na mtu mwingine."


Alisema kutoa maoni ni haki ya kila mtanzania ambayo amepewa kikatiba ili mradi asivunje sheria, na kuongeza kuwa Kitine ametumia haki yake ya kikatiba.


"Kila mtanzania ana haki ya kutoa maoni ili mradi asivunje sheria," alisema Msekwa.


Aliongeza kuwa kwa maoni yake binafsi CCM haitazungumzia maoni ya mtu binafsi na wala si utaratibu mzuri kwa viongozi kuzungumzia na kutolea kauli maoni ya watu.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...