Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri cha Serikali ya Awamu ya Sita kilichofanyika tarehe 14 Julai, 2025 katika Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.
Mara baada ya kikao hicho, Rais Dkt. Samia alipiga picha ya pamoja na viongozi wakuu wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko, pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Mheshimiwa Balozi Dkt. Moses Kusiluka, sambamba na Mawaziri wote waliokuwepo.
Picha hiyo ya pamoja ni kumbukumbu muhimu ya kipindi cha mwisho cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita kabla ya kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ambapo Watanzania watapata fursa ya kuamua uongozi wa awamu inayofuata.
Kikao hiki kimeweka alama ya hitimisho la muhula wa uongozi ambao umetajwa kuwa wa mageuzi na mafanikio katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Ni fursa ya kutathmini yaliyofanikishwa, kujifunza kutokana na changamoto, na kujiandaa kwa hatua zinazofuata kwa mustakabali wa taifa.
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuonesha mshikamano, weledi na dhamira ya dhati katika kuwatumikia wananchi kwa misingi ya uwazi, uwajibikaji na maendeleo jumuishi.
No comments:
Post a Comment