Thursday, July 17, 2025

RAIS SAMIA AZINDUA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

 




















Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC), jijini Dodoma, tarehe 17 Julai 2025.

Dira hii ni mwongozo wa kitaifa unaolenga kuelekeza juhudi za maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiteknolojia kwa kipindi cha miaka 25 ijayo, ili kuhakikisha Tanzania inakuwa taifa lenye ustawi wa watu wake na uchumi imara.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa, sekta binafsi, wadau wa maendeleo na wananchi, ikiwemo Mwenyekiti Mstaafu wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe, aliyesalimiana na Rais Samia mara baada ya uzinduzi huo – ishara ya mshikamano na mshirikiano katika utekelezaji wa dira hii.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais Samia alisisitiza kuwa Dira ya 2050 inalenga kujenga uchumi wa kisasa unaotumia teknolojia, kuimarisha miundombinu, kuongeza ajira, na kukuza ubora wa maisha ya Watanzania wote.

Dira hii imebuniwa kwa kushirikisha wadau kutoka sekta zote, na utekelezaji wake utahusisha mikakati madhubuti katika nyanja za elimu, afya, viwanda, mazingira na utawala bora.

#Tanzania2050 #MaendeleoYaTanzania #DiraYa2050 #JKCCDodoma #RaisSamia #KujengaTaifa


No comments:

RAIS SAMIA AZINDUA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , amezindua rasmi Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi w...