Saturday, July 05, 2025

RAIS DKT. SAMIA AZINDUA KANISA LA ARISE AND SHINE, KAWE – AWAPUNGIA WAUMINI KWA SHUKRANI















Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 5 Julai 2025, amehitimisha hafla ya uzinduzi wa Kanisa la Arise and Shine lililopo Kawe, Jijini Dar es Salaam kwa hotuba maalum iliyojaa faraja, matumaini na wito wa kuimarisha maadili ya kiroho katika jamii.

Katika hotuba yake mara baada ya kulizindua rasmi kanisa hilo, Mhe. Rais Dkt. Samia aliwahimiza viongozi wa dini na waumini kuendelea kulieneza neno la Mungu kwa njia ya amani, mshikamano na upendo kwa taifa zima. Aidha, alilitaja kanisa kama kiungo muhimu katika kujenga jamii yenye maadili na moyo wa kusaidiana.

Baada ya hotuba hiyo, Rais Dkt. Samia aliwaaga waumini waliohudhuria tukio hilo la kihistoria kwa kuwapungia mkono kwa bashasha, ishara ya upendo na mshikamano na watu wa Kawe na Tanzania kwa ujumla.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini, pamoja na waumini wa madhehebu tofauti waliokuja kushuhudia tukio hilo muhimu la kiimani.

No comments:

NHC YAKABIDHI MSAADA KWA WATU WENYE ULEMAVU UBUNGO

  Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kupitia kwa Afisa wake Mkuu wa Habari, Yahya Charahani, limekabidhi msaada wa vifaa vya kusaidia watu we...