Mkuu wa Mkoa wa Iringa Komred Kheri James amewaongoza viongozi na watumishi wa mkoa huo katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa wawekezaji na wafanyabiashara mkoani humo kwa lengo la kutambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na kundi hilo kubwa mkoani Iringa.
Akizungumza katika hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa na kuhudhuriwa na Wawekezaji na Wafanyabiashara kutoka wilaya zote za Mkoa wa Iringa, Komred Kheri James ameeleza kuwa Serikali imeona ni vyema kutoa Tuzo na pongezi hizo ili kuongeza, kutambua, kuthamini na kutangaza kazi kubwa inayo fanywa na Wawekezaji hao katika kutengeneza ajira, kutoa huduma kwa Wananchi, kuchangia mapato ya Serikali imeona ni vyema kutoa Tuzo na pongezi hizo ili kuongeza, kutambua, kuthamini na kutangaza kazi kubwa inayo fanywa na Wawekezaji hao katika kutengeneza ajira, kutoa huduma kwa Wananchi, kuchangia mapato ya Serikali na kusaidia kukuza miji na huduma.
Pamoja na mambo mengine, Komred Kheri James ameeleza kuwa Serikali itaendelea kutengeneza mazingira bora ya biashara ilikukuza uchumi wa mtu moja moja na kufungua zaidi fursa za uwekezaji kwa faida ya Umma.
*#Iringa Imara, Tutaijenga kwa Umoja na Uwajibikaji*
No comments:
Post a Comment