Monday, July 14, 2025

BALOZI NCHIMBI AONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU TAIFA DODOMA




Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akiongoza kikao cha kawaida cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, leo Julai 14, 2025 katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM (White House) mkoani Dodoma.

Kikao hicho, kinachotarajiwa kuendelea hadi Julai 16, kimeitishwa kufuatia kukamilika kwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi wa nafasi za uwakilishi katika vyombo vya dola. Nafasi hizo zinahusisha ubunge wa majimbo, ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, viti maalum vya ubunge na Baraza la Wawakilishi, pamoja na udiwani wa kata na viti maalum.

No comments:

TRENI YA MWENDOKASI KUFIKA MWANZA 2028

  Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kutoka kulia),akizungumza baada ya kukagua daraja la kupitisha magari chn ya reli, l...