Saturday, July 05, 2025

HALMASHAURI ZATAKIWA KUSIMAMIA UENDELEVU WA MATOKEO BORA KWA WANUFAIKA WA MRADI






Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Amina Mfaki amezitaka Halmashauri za Wilaya ya Chamwino, Halmashauri ya Wilaya Manyoni na Halmashauri ya Wilaya ya Singida kuweka mikakati thabiti ya kuendelea kulea kaya na vikundi mbalimbali vilivyokuwa vikisimamiwa kupitia Mradi wa kusaidia Kaya Masikini na kaya zenye watu wenye ulemavu kutoka shirika la BRAC Maendeleo ambao umefika mwisho.

Bi. Amina ameyasema hayo Katika kikao cha kufunga Mradi wa  kusaidia kaya Masikini na kaya zenye watu wenye ulemavu kutoka shirika la  BRAC Maendeleo ambao umekuwa ukihudumia watu wenye ulemavu na Kaya zisizo na uwezo katika Halmashauri hizo Wilayani Chamwino, mkoani Dodoma.

“Tumeona namna gani wameweza kuwainua watu wa Kaya zisizo na uwezo na watu wenye ulemavu, hivyo tunatarajia baada ya BRAC Maendeleo kumaliza muda wao ni jukumu la Halmashauri zote kuendelea kusimamia zile kaya na watu wote ambao walikuwa ni wanufaika wa Mradi"

Naye, Meneja wa Mradi wa kusaidia kaya masikini na kaya zenye watu wenye ulemavu kutoka shirika la BRAC Maendeleo Bi. Rachel Bwiliza ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ushirikiano mkubwa katika kufanikisha mradi huo.

Amesema mradi huo umetekelezwa Kwa kipindi cha miezi 30 na umekekezwa katika Mikoa ya Dodoma na Singida katika Halmashauri tatu na kufanikiwa kuwahudumia wahitaji zaidi ya  1,050 ambapo 85% kati ya hao ni kaya zinazoongozwa na wanawake wenye kipato cha hali ya chini huku 15% ikiwa ni kaya za watu wenye ulemavu

No comments:

MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. MPANGO ASHIRIKI MISA YA UPADIRISHO NA UFUNGUZI WA MWAKA WA JUBILEI YA MIAKA 50 KIWANJA CHA NDEGE, DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ameungana na waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa Kanis...