Maswa, Simiyu – 18 Juni 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amehutubia maelfu ya wananchi wa wilaya ya Maswa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoani Simiyu.
Katika hotuba yake, Mhe. Rais Samia amewaeleza wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika nyanja za elimu, afya, barabara, kilimo na viwanda, akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kupeleka huduma bora kwa wananchi wote bila ubaguzi.
Akiwahamasisha wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali, Mhe. Rais amesisitiza umuhimu wa mshikamano, amani na utulivu kama nguzo muhimu ya maendeleo ya Taifa.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na wananchi wa Maswa na maeneo jirani, ambapo shangwe na vifijo vilitawala uwanja huo ikiwa ni ishara ya mapokezi makubwa kwa kiongozi huyo wa nchi.

No comments:
Post a Comment