Tuesday, May 31, 2016

MKE WA RAIS MAMA JANETH AWATAKA WATANZANIA KUWASAIDIA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkaribisha Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa Ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam. Mama Majaliwa alifika Ofisini hapo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na mke wa Rais.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli Magogoni jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimuonesha Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa mafuta maalumu yanayotumiwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino ambayo atayagawa hivi karibuni kwa baadhi walemavu wa ngozi katika maeneo mbalimbali nchini. Pia Mke wa Rais mama Janeth amewaomba watanzania kuwajali Wazee na watu wenye ulemavu wa ngozi. PICHA NA IKULU.

BALOZI HERBERT MRANGO AKAGUA UKARABATI MV MAGOGONI

 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Silvester Simfukwe (katikati walio chuchumaa) akiwaonesha Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) sehemu ya kivuko cha Magogoni inayoendelea kufanyiwa ukarabati.
Kivuko cha Magogoni kikiwa katika ukarabati katika Bandari ya Dar es Salaam.Picha na Theresia Mwami-TEMESA.
 Kaimu Mtendaji wa TEMESA Mhandisi Manase Ole kujan (Kushoto) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Balozi Herbert Mrango (katikati) wakati Bodi hiyo ilipotembele ukarabati wa kivuko cha magogoni.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Balozi Herbert Mrango( wa tatu kulia) akiongoza na wajumbe wa bodi hiyo wakati Bodi hiyo ilipotembele ukarabati wa kivuko cha magogoni.
Na Theresia Mwami- TEMESA

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imetembelea na kujionea maendeleo ya ukarabati wa kivuko cha Mv Magogoni chini ya kampuni ya Songoro Marine katika Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Balozi Herbert Mrango ameeleza kuridhishwa na kasi ya ukarabati wa kivuko hicho na kuushauri uongozi wa TEMESA kuharakisha malipo yanafanyika kwa wakati ili kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa.

“Nakuagiza Kaimu Mtendaji uhakikishe malipo kwa kampuni hii yanafanywa kwa wakati na ukarabati huu kukamilika mapema ili kuwapa fursa wananchi kutumia kivuko hiki”alisema Balozi Mrango.

Aliongeza kuwa ni muhimu wananchi kurejeshewa huduma ya kivuko hicho ili kuondoa kero inayowakabili kwa sasa kwa kuwa na kivuko kimoja chenye uwezo wa kubeba magari ambapo kukamilika kwa ukarabati wa huu utakuwa umerahisiha shughuli ya usafirishaji.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji wa TEMESA Mhandisi Manase Ole kujan amesema atahakikisha malipo yanafanyika kwa wakati ili kuwezesha mkandarasi huyo kumaliza kazi hiyo kwa muda uliopangwa na kurejesha huduma ya kivuko hicho kwa wananchi.

Aidha aliongeza kuwa kazi ya ukarabati wa kivuko hicho imegawanywa katika sehemu mbili ambazo ni, ukarabati wa “Body” pamoja na mifumo ya umeme unaofanywa na Mkandarasi kutoka kampuni ya Songoro Marine huku TEMESA ikihusika na ukarabati wa mitambo ya kuongozea kivuko.

Kivuko cha Mv Magogoni kinachotoa huduma katika maeneo ya kigamboni na Magogoni Jijini Dar es Salaam kilisimamisha rasmi kutoa huduma hiyo mapema Mei mwaka huu kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati mkubwa chini ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na kampuni ya Songoro Marine kukiongezea ufanisi katika kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi.

LUHWAVI AKAGUA JENGO LA MIKUTANO LA CCM DODOMA LEO

Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi hali ya maua kwenye bustani za jengo hilo, alipokagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu. 
Luhwavi akielekeza namna ya kuboreshwa bustani zinazozunguka jengo la ukumbi huo 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akizunguka jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Cetre, alipokagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu
Luhwavi akiingia ndai ya ukumbi wa jengo hilo kuona hali halisi 
Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison (kushoto), akimpa maelezo kuhusu hali ya ndani ya jengo hilo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipolikagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu. 
Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison (kushoto), akionyesha baadhi ya viti ambayo hutumiwa na wajumbe, katika ukumbi huo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (hayupo katika picha), alipolikagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu. Mkuu wa Idara ya Usalama na Maadili Makao Makuu ya CCM, Masudi Mbengula 
Bendera ya Taifa na bendera ya CCM zikipepea kwenye jengo hilo la Mikutano la CCM, kama ilivyo kawaida.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi (wapili kushoto) akikagua jengo la Mikutano la CCM, Dodoma Convetion Centre leo ikiwa ni maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai mwaka huu katika ukumbi huo. Kushoto ni Ofisa Miliki wa Jengo hilo Tegemeo Saambili 

Luhwavi akitazama hali ya maua kwenye bustani za jengo la ukumbi huo 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Tegemeo Saambili (kushoto), alipokagua jengo hilo leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akihoji kuhusu hali ya bustani zinazozunguka jengo hilo 

Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi hali ya maua kwenye bustani za jengo hilo, alipokagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu. 
 PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KATIKA HAFLA YA UTOAJI WA TUZO ZA RAIS KWA WAZALISHAJI BORA WA VIWANDA KWA MWAKA 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na washindi mbalimbali waliopata tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa viwanda kwa mwaka 2015. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo mpya ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa Viwanda  PMAYA The President’s Manufacure of the Year  pamoja na Mwenyekiti wa Wenyeviwanda Tanzania CTI Dkt. Samwel Nyantahe katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wadau mbalimbali wa CTI na kutoka Sekta ya Viwanda nchini kabla ya kutoa Tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2015 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Leodgar Tenga mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wadau wa Viwanda nchi mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.
PICHA NA IKULU.

MAADHIMISHO YA MWAKA MMOJA WA GYM NHC AMBAYO YALIAMBATANA NA KUMUAGA MWANA GYM TIMON MANONGI

Kikosi cha mazoezi cha Shirika la Nyumba la Taifa kikiwa katika picha ya pamoja kwenye Bustani ya Jengo la Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa kuanzishwa kwa GYM kwajili ya kujiweka sawa afya za miili yao.
Kikosi cha mazoezi cha Shirika la Nyumba la Taifa kikiwa katika picha ya pamoja kwenye Bustani ya Jengo la Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa kuanzishwa kwa GYM kwajili ya kujiweka sawa afya za miili yao.
Kikosi cha mazoezi cha Shirika la Nyumba la Taifa kikiwa katika picha ya pamoja ndani ya GYM ya Jengo la Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC PLACE kikikongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Baadaye kikosi hicho cha mazoezi cha Shirika la Nyumba la Taifa kilihamia katika ukumbi maarufu wa burudani wa Rhapsody kwaajili ya hafla ya pamoja ya maadhimisho ya mwaka mmoja lakini pia kumuaga mmoja wa wanachama wa GYM, Timon Manongi ambaye anaondoka kwenda masomoni.
 Baadaye kikosi hicho cha mazoezi cha Shirika la Nyumba la Taifa kilihamia katika ukumbi maarufu wa burudani wa Rhapsody kwaajili ya hafla ya pamoja ya maadhimisho ya mwaka mmoja lakini pia kumuaga mmoja wa wanachama wa GYM, Timon Manongi ambaye anaondoka kwenda masomoni.
Aliyekuwa Msimamizi wa Miradi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Timon Manongi akipewa mkono wa heri na Mkurugenzi wa Ubunifu ambaye ni bosi wake katika hafla ya kumuaga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Rhapsody.
Aliyekuwa Msimamizi wa Miradi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Timon Manongi akifurahia zawadi yake aliyopewa na Mkurugenzi wa Ubunifu ambaye ni bosi wake katika hafla ya kumuaga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Rhapsody.
 Aliyekuwa Msimamizi wa Miradi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Timon Manongi akifurahia zawadi yake ya keki aliyopewa na wafanyakazi wenzake.
  Aliyekuwa Msimamizi wa Miradi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Timon Manongi akifurahia zawadi yake ya keki aliyopewa na wafanyakazi wenzake.
 Aliyekuwa Msimamizi wa Miradi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Timon Manongi katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake.
  Aliyekuwa Msimamizi wa Miradi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Timon Manongi katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake.
 Mwalimu wa mazoezi wa GYM ya NHC akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wake katika picha ya pamoja kwenye ukumbi wa Rhapsody mwishoni mwa wiki.
 Mwalimu wa mazoezi wa GYM ya NHC akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wake katika picha ya pamoja kwenye ukumbi wa Rhapsody mwishoni mwa wiki.


BUNGE LAWASIMAMISHA WABUNGE KWA KUFANYA VURUGU BUNGENI JANUARI 27 ,2016

IMG-20160530-WA0066

Monday, May 30, 2016

RAIS MAGUFULI ATEUA JAJI WA RUFANI, MWENYEKITI WA NHIF NA MWENYEKITI WA DIT

Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi huo Mhe.  Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi.
Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Mhe. Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).Uteuzi wa Mhe. Anne Semamba Makinda  ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza tarehe 25 Mei, 2016.

Mhe. Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo.Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es salaam Institute of Technology - DIT).

Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro.Prof. Pereka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

30 Mei, 2016

YALIYOJILI KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO LEO MJINI DODOMA

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Mwansasu akiongoza kikao cha 32 cha Mkutano wa tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
  Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa  
kikao cha 32 cha Bunge hilo mjini Dodoma
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla akijibu maswali ya wabunge kuhusu sekta ya Afya Bungeni mjini Dodoma.
 Mbunge wa jimbo la Ukonga (CHADEMA) Mhe. Mwita Mwikwabwe akisoma kitabu cha Kanuni za Kudumu za Bunge ndani ya Ukumbi wa Bunge.
  Mbunge wa Nzega Mhe. Hussein Bashe (CCM) akizungumza jambo na Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kulia) nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha 32 cha mkutano wa tatu wa Bunge leo mjini Dodoma.
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari Barbro Johansson iliyoko jijini Dar es salaam wakiondoka ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Sulemani Jafo akijibu maswali ya wabunge yaliyoelekezwa kwenye wizara yake Bungeni mjini Dodoma.
 Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge kufuatia Naibu Spika wa Bunge hilo Mhe. Tulia Ackson kutangaza kuliahirisha Bunge leo mjini Dodoma.

 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba nje ukumbi wa Bunge.
 Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akizungumza jambo na wabunge leo mjini Dodoma.
 Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
  Mbunge wa Kigoma Mhe. Peter Selukamba akijadiliana jambo na  Mbunge wa Nzega mjini Mhe. Hussein Bashe (kushoto)Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu nje ya Ukumbi wa Bunge mjini.
Kikao cha 32 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asubuhi.
 Wabunge wakiondoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya Naibu Spika kutangaza kuahirisha shughuli za Bunge leo.
 Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. PICHA/Aron Msigwa na Fatma Salum - DODOMA.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...