Thursday, October 01, 2015

AIRTEL YATOA GAWIO LA TSHS BILIONI 5.3 KWA WATEJA WA AIRTEL MONEY


Meneja biashara wa kitengo cha  Airtel Money,  Bwn Asupya Naligingwa
(kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza Airtel
kugawa gawio la faida la zaidi ya  shilingi billion 5 kwa wateja na
mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money nchi nzima.  Pichani
ni Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Bi Jane Matinde

KAMPUNI ya simu za mkononi
ya Airtel leo imetangaza kugawa zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa wateja
na mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money nchi nzima

Uamuzi huo wa kutoa gawio la faida lililopo katika akaunti  ya
udhamini ya wateja wa Airtel Money (Trust account)  litawawezesha
wateja wa Airtel kulipwa kiwango kizuri cha gawio la faida.  Kiwango
hiki cha pesa kitalipwa kutokana na  kiasi cha pesa mteja alichokuwa
nacho kwenye akaunti yake ya Airtel Money kila mwisho wa siku  kuanzia
March 2014 hadi April 2015.

Akiongea na waandishi wa habari,Meneja wa kitengo cha  Airtel Money,
Asupya Nalingigwa, alisema wanayo furaha kutangaza mgawanyo  huu wa
gawio la faida kwa wateja wao baada ya benki kuu ya Tanzania.
Kuidhinisha kutoa  pesa hizi katika akaunti ya udhamini ya pesa za
wateja wa Airtel Money ijulikanayo kama trust  account.

Aliongeza kwa kusema wateja wa Airtel Money watapata sehemu ya gawio
lao  kulingana na salio wanalokuwa nalo kwenye akaunti zao kila siku

"Tunaamini kiasi hiki cha pesa kitachangia kwa kiasi kikubwa katika
kuboresha maisha ya watanzania wengi , kuwahamasisha wateja
wasiofikiwa na huduma za kibenki kutumia mfumowa pesa kwa njia ya
simu.Vilevile wateja wetu wa Airtel Money wataendelea kutumia huduma
za pesa kupitia simu za mkononi, kufanya miamala yao ya kila siku na
kutunza pesa zao ili kupata gawio lao kila watakapo weka pesa katika
akaunti zao za Airtel Money". Aliongeza Nalingigwa

Uamuzi huu wa kutoa gawio la faida kwa wateja ni wakuungwa mkono kwani
unachochea na kuboresha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu za
mkononi , ukizingatia takribani asilimia 85% ya watanzania bado
hawajafikia na huduma za kibenki

Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma za kibunifu  za
kifedha kupitia simu za mkononi ikwemo NFC huduma inayokuwezesha
kufanya malipo kupitia kadi, Mikopo ya Timiza na huduma nyingine
nyingi.

Katika  maelezo yake Naligingwa aliahidi  Airtel kuendelea na dhamira
yake ya kuzindua huduma bora na za kisasa katika mienzi ijayo ili



kuwanufaisha watanzania waishio maeneo ya mijini na vijijini.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...