Thursday, October 15, 2015
MWENYEKITI MWENZA WA UKAWA, EMMANUEL MAKAIDI AFARIKI DUNIA
WASIFU WA MAREHEMU KWA UFUPI:Dk Emmanuel Makaidi alikuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NLD na ni mhandisi aliyebobea. Alizaliwa Aprili 10, 1941 huko wilayani Masasi mkoani Mtwara. Baba yake mzazi alikuwa ni katekista wa Kanisa la Anglikana.
Alianza elimu katika Shule ya Msingi Namalenga wilayani Masasi kati ya mwaka 1948 – 1952, mwaka 1953 – 1954 alisoma katika Shule ya Kati (Middle school) iitwayo Luatala hukohuko Masasi. Baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari ya Chuo cha Mtakatifu Joseph na kusoma kidato cha kwanza hadi cha nne kati ya mwaka 1953 hadi 1956.
Makaidi alisoma darasa la 13 na 14 (kidato cha tano na sita) katika Shule ya Sekondari Luhule, Uganda kati ya mwaka 1957 – 1958. Alipelekwa Uganda si kwa sababu ya kipato cha baba yake, la hasha, alisaidiwa na Askofu wa Anglikana baada ya kuona anafaulu mitihani yake kwa alama za juu sana.
Makaidi aliendelea kufadhiliwa na askofu huyo ambaye alimuunganisha na mashirika mengine na kumtafutia chuo Afrika ya Kusini. Akapelekwa Chuo Kikuu cha Witwatersrand na kuhitimu Shahada ya Uendeshaji na Usimamizi kati ya mwaka 1958 – 1960.
Baada ya kuhitimu vizuri pale Witts, aliendelea kupata ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili, mara hii alielekea Marekani na kusoma masuala ya Menejimenti na Utawala kwa ngazi ya uzamili kati ya mwaka 1960 – 1962. Alisoma pia katika Chuo Kikuu cha Howard kilichoko jijini Washington, Marekani.
Baada ya kurejea nchini akiwa mhitimu wa M.A, Makaidi alianza kazi serikalini mwaka 1966 hadi mwaka 1973 akiwa mchambuzi kazi mkuu, katika kitengo cha Utumishi.
Kati ya mwaka 1974 na 1975 (miaka miwili). Alirudi tena Marekani na kusoma Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Howard akipata kuwa karibu na mmoja wa maprofesa nguli duniani, Wamba Dia Wamba. Makaidi ameniambia kuwa hata tabia ya kuandika vitabu na kutunga mambo ya ubunifu, alifundishwa na profesa huyu mahiri.
Aliporejea nchini kwa mara ya pili mwaka 1976 aliendelea na kazi yake pale Utumishi hadi mwaka 1985 alipopewa kazi nyingine kubwa zaidi, akawa Mkurugenzi wa Miundo na Mishahara kwenye kamati iliyokuwa inashughulikia mashirika ya umma nchini.
Wakati anaendelea na kazi utumishi, alipata fursa nyingine ya kusomea stashahada ya Kuchakata Taarifa za Kielektoniki katika Chuo Kikuu cha Trinity, Ireland. Alikwenda huko na kuhitimu mwaka huohuo 1977.
Kabla hajafanya kazi katika kamati maalum ya kusimamia mashirika ya umma akapandishwa cheo na kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ustawi wa Jamii na mwaka huohuo 1985 akafukuzwa kazi.Kisa cha Makaidi kufukuzwa kazi serikalini, tena akiwa na wadhifa huo ilikuwa ni kwa sababu ya kuandika kitabu cha Kiingereza chenye jina “mwanasiasa mwenye roho ya shetani”. Serikali ikamzonga vilivyo, ikamtuhumu kuwa kitabu kile kinamtukana Mwalimu Julius Nyerere. Mwisho wa siku “kazi ikaota mbawa”.
Bahati nzuri, mwaka huohuo 1985 akaajiriwa na Shirika la Finwork Directory kuwa Mkurugenzi Mtendaji, kazi aliyoifanya hadi mwaka 1991.
Kuanzia mwaka 1992 hadi mauti yanamkuta, Dk Makaidi hakujishughulisha tena na kazi za serikalini wala mashirika binafsi. Alijiajiri akiwa na kampuni kadhaa zilizoajiri Watanzania wa vipato vya kawaida, lakini pia aliendelea kutoa ushauri wa kitaalamu kwa kampuni za ndani na nje ya nchi huku akiongoza chama cha NLD akiwa Mwenyekiti.
Dk Makaidi alikuwa mwandishi mzuri wa vitabu, alishaandika zaidi ya 10. Amemuacha mjane Modesta Ponela na watoto wanane.
SOURCE:JAMIIFORUMS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment