Friday, October 16, 2015

FLY OVER YA TAZARA KUPUNGUZA FOLENI KWA KIASI KIKUBWA

 Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya zoezi la utiaji wa saini wa ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya Tazara (Flyover).
Waziri wa Ujenzi Dk,John Magufuli jana ametia saini na mkandarasi wa Japani tayari kwa kuanza ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la  Tazara jijini Dar es Salaam.
Dkt,Magufuli akizungumza na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam hususani Jimbo la Ukonga  kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Moshibar Mombasa, katika wilayan ya  Ilala alisema kuwa baada ya  kuunganisha ujenzi wa barabara za mikoa  na Wilaya sasa nguvu zake zinaelekeza kukabiliana na  mkakati wa kuondoa foleni.
Alisema kuwa katika kuhakikisha wanamaliza tatizo hilo katika jiji la Dar Salaam juhudi za kujenga barabara za juu zinaendelea na tayari Serikali  imeshapata fedha ambazo zitajenga barabara hiyo  (flyover) kwenye  makutano ya ya mataa ya Tazara.
Akitoa ufafanuzi huo kwa wananchi ambao walijitokeza kwa wingi katika mkutano wake alisema  kuwa (jana ) yaani juzi amesaini mkataba wa kuaza ujenzi wa barabara hiyo ya njia saba, ambapo kukamilika kwake kutasaidia kupunguza tatizo la foleni.
“Nakwenda kusaini mkataba wa kuanza ujenzi wa (flyover) kwenye makutano ya tazara,na fedha zimekwishaingia mkandalasi ameshapatikana wa Japani tayari kuaza ujenzi wa barabara hiyo.”alisema.
Aliongeza kuwa mbali na eneo hilo la Tazara pia Serikali imeshapata fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze kwa sh.trioni 2.4 na daraja kubwa kutoka Salenda bridge kuzunguka Cocobeach zaidi ya bilioni 200,zimeshapatikana.
Aidha alisema daraja la kigamboni mita 60 linatarajia kukamilika muda mfupi ujao hivyo likisha kamilika na kukamilika kwa njia hizo kwa kiasu kikubwa kutamaliza foleni jiji la Dar es  Salaam
 Zoezi la utiaji saini likiendelea.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...