Sunday, October 25, 2015

MTONI KIJICHI, MBAGALA WENGI WAJITOKEZA KUPIGA KURA KWA UTULIVU NA AMANI JIJINI DAR ES SALAAM

 Rukia Omari (kushoto), akimsaidia kupiga kura jamaa yake Mwanaharusi Mohamed ambaye ni mlemavu wa macho wakati wa kupiga kura katika kituo cha Mbagala Misheni Dar es Salaam leo asubuhi.
  Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika Kituo cha Mtoni Kijichi Stendi Dar es Salaam leo asubuhi.
 Wananchi wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Shimbwe Mbagala Kuu.
 Hapa wakihakiki majina yao.
 Mkazi wa Njia ya Ng'ombe Mbagala Kuu, Sarah Simba akipiga kura katika kituo cha Shimbwe Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kuwachagua viongozi wake, Rais, Mbiunge na Diwani.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya kwenda kupiga kura katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mbagala Kuu.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Bwawani Mtoni Kijichi leo asubuhi.
 Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika Kituo cha Mtoni Kijichi Stendi Dar es Salaam leo asubuhi.

 Wasimamizi wa uchaguzi katika kituo cha Mbagala Misheni wakiwa kazini.
Msimamizi wa uchaguzi Mkuu katika kituo cha Mbagala Misheni, Yona Komba (kulia), akimpaka winoMwanaharusi Mohamed ambaye ni mlemavu wa macho baada ya kumaliza kupiga kura katika kituo hicho Dar es Salaam  leo asubuhi. Kushoto ni binti aliyemuomba amsaidie kupiga kura  Rukia Said.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...