Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji Damian Lubuva akifafanua baadhi ya mambo mapema leo jioni kabla ya mawakala wa vyama kusaini fomu namba 27 iliyosainiwa na mawakala wa vyama vya siasa baada ya majumuisho ya kura kwa wagombea urais kabla ya kutangaza rais mteule wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo Dk. John Pombe Magufuli ametangazwa mshindi kwa kura kura 8.882.935 sawa na asilimia 58.46 huku mpinzania wake kutoka Umoja wa Vyama vya Upinzani kupitia chama cha Chadema Edwald Lowasa akipata kura 6.072.848 sawa na asilimia 39.97.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji Damian Lubuva akisaini fomu namba 27 mara baada ya mawakala wa vyama vya siasa kusaini kabla ya kumtangaza rasmi rais mteule kwenye ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam leo ambapo Dk. John Pombe Magufuli ametangazwa kuwa rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushoto ni Mkurugenzi wa Tume hiyo Ndugu Kailima Ramadhan na kushoto ni Jaji Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmod Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM nakala ya fomu namba 27 ambayo mawakala wa vyama wamesaini mara baada ya kukamilisha majumuisho ya kura za wagombea urais kabla ya kutangaza matokeo mapema leo katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Hamid Mahmod.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Jaji Damian Lubuva akitangaza matokeo hayo kwenye ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya mawakala na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa waliohudhuria kushuhudia matangazo hayo yaliyokuwa yakitolewa na tume ya uchaguzi ya taifa leo kwenye ukumbi wa kimataifa wa JNICC jijini Dar es salaam.
Maofisa mbalimbali wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na serikali wakifuatilia matangazo hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na wageni mbalimbali wa ndani na nje waliohudhuria ili kushuhudia Rais mteule akitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Assa Mwambene Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali TSM Gabriel Nderumaki wakijadili jambo wakati wakisubiri kuanza kwa utiaji saini kwa mawakala wa vyama vya siasa kwenye fomu namba 27 kabla ya kutangaza matokeo ya jumla ya wagombea urais wa Tanzania.
Baadhi ya mawakala wakipitia fomu namba 25 na 26 kabla ya kusaini fomu namba 27.
Baadhi ya mawakala wakisaini fomu hizo.
No comments:
Post a Comment