Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akipokea wageni nyumbani kwake kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa jijini Dar.
(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (katikati) akimtambulisha mmoja wa wageni waalikwa kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kulia).
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini, Joyce Mends-Cole (kulia) akifurahi jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kushoto) wakati wa zoezi la kupokea wageni waalikwa kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Tanzania. Katikati ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.
Wageni mbalimbali wakiendelea kuwasili na kupokelewa na wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez (kushoto) akiongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim mara tu alipowasili kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kulia) akifurahi jambo na mmoja wa wageni waalikwa. Katikati ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.
Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy pamoja na Katibu wa Dkt. Mahadhi wakiwa kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisherehesha mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Tanzania, nyuma yake ni wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa Tanzania.
Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez wakitazama moja ya ‘Documetary’ ya Malengo Endelevu ya dunia katika mnuso wa birthday ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Msaidizi wa Mh. Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Hoyce Temu na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Naibu Waziri huyo.
No comments:
Post a Comment