Wednesday, October 14, 2015

MAGAVANA WA AFRIKA WAKUTANA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA KUJADILI NAMNA YA KUCHOCHEA MAENDELEO

x1

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile wakisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde wakati akiingia kwenye ukumbi wa mkutano.
x2
Katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde akinukuu hoja zilizokuwa zikijadiliwa katika mkutano huo.
x3
Wa pili kulia ni Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi Benki Kuu ya Tanzania Dr. Joseph Masawe.
x4
Ujumbe wa Tanzania wakiwa kwenye mkutano wakujadili namna ya kuimarisha uchumi na kuchoche maendeleo Barani Afrika. Kutoka kushoto ni Kamishna Idara ya Sera Bw. Bedason Shallanda, Mhasibu Mkuu Msaidizi Bw. Ishmael Kasekwa, John Mavura mchumi Wizara ya Fedha na Bw. Patrick Pima mchumi Wizara ya Fedha.
x5
Magavana wa Afrika wakiwa kwenye Mkutano wa majadiliano na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde na Rais wa Kundi la Benki ya Dunia Dr. Jim Yong Kim nchini Peru – Lima.
Imetolewa na
Msemaji wa Wizara ya Fedha
Bi. Ingiahedi Mduma
13/10/2015

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...