Wednesday, October 14, 2015

PSPF YAVUNA WANACHAMA KUTOKA KIKUNDI CHA WAJASIRIAMALI WA VOWET

Meneja wa Mfuko wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, (aliyesimama), akiwaongoza wanachama wapya waliojiunga na mpango huo, wakati wa warsha ya siku moja iliyowakutanisha maafisa na mabalozi wa PSPF, na wanakikundi wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania, (VOWET), kwenye ukumbi wa Belmonte jijini Dar es Salaam, Oktoba 13, 2015. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Na K-VIS MEDIA
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umezidi k”kupenya’ kwenye sekta binafsi na kuvuna wanachama zaidi kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, ambapo wanakikundi wajasiriamali wa kundi la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (Voice of Women Entrepreneurs Tanzania-VOWET).
Wanachama hao wapya walijiunga baada ya kushiriki warsha ya siku moja ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa Belmonte ulioko jingo la makao makuu ya PSPF, jijini Dar es Salaam Oktoba 13, 2015, ambapo Mabalozi wa Mfuko huo, Msanii wa majigambo, Mrisho Mpoto na Mwanamitindo wa Kimataifa anayeishi na kufanyia kazi zake jijini New York Marekani, Flaviana Matata, walishiriki kutoa “Darasa” kuhusu umuhimu wa Watanzania walio katika sekta bionafsi kuchangamkia fursa kupitia kuiunga na uamancaha wa Mfuko huo kupitia mpango wa PSS.
Mabalozi hao waliongozwa na Meneja wa Mpango wa PSS, Mwanjaa Sembe, na Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko huo, Magire Werema, ambao wote kwa pamoja walifafanua na kueleza kwa kina faida za kuwa mwanachama wa Mfuko huo, ambapo kwa muda mfupi baada ya kujiunga Mwanachama anawezakufaidi mafao mbalimbali yatolewayo na Mfuko huo ikiwemo mikopo ya nyumba, Fao la Elimu, na mengine mengi.
Kufuatia :Darasa” hilo, wanachama wa VOWET walijiunga na Mfuko huo kupitia mpango wa PSS
 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, akitoa mada
 Magire Werema, Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF
 Balozi wa PSPF, Mwanamitindo wa Kimataifa aishie nchini Marekani, Flaviana Matata
 Balozi wa PSPF, Msanii maarufu Tanzania, Mrisho Mpoto akitoa mada
 Mjumbe wa Bodi ya Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania, VOWET, Anne A. Ottieno, akiuliza swali
 Wanachama wa VOWET, wakijaza fomu za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari PSS, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakat wa Warsha hiyo
 Mwanachama wa VOWET, akijaza fomu tayari kuwa Mwanachama wa PSPF, kupitia mpango wa PSS
 Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Rahma J Ngassa, (kushoto), akiteta jambo wa Balozi wa Mfuko huo, Flaviana Matata
 Rahma akiteta jambo na Meneja wa Flaviana Matata, Shamim Mwasha(kulia)
 Meneja wa Mpango wa PS, Mwanjaa Sembe, (kushoto), akimsikiliza Mjumbewa Bodi ya VOWET, Anne Ottieno wakati akijiandaa kujaza fomu za kujiunga na Mpango huo


 Flaviana (wapili kulia), akiwaelekeza wanachama wa VOWET, jinsi ya kujaza fomu za kujiunga uanachama.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...