Maafisa wa Bunge wakibebea Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, wakati ulipowasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam Oktoba 15, 2015 kwa ajili ya kuagwa.
Picha na OMR
Spika wa Bunge Mama Anne Makinda, akizungumza kutoa salamu kwa niaba ya Bunge.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu, kumswalia Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, wakati wa swala hiyo iliyoswaliwa kwenye Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo Jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo Jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo Jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga.
Baadhi ya Wanafamilia wa marehemu Dkt. Kigoda.
Sehemu ya waombolezaji na Wabunge waliohudhuria shughuli hiyo ya msiba Karimjee.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakijumuika na baadhi ya biongozi wa Kitaifa na Waombolezaji, kushiriki katika shughuli ya kuagwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, iliyofanyika leo Okt. 15, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakary Zubeiry, wakati alipowasili kwenye Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam, leo asubuhi kwa ajili ya kuswalia mwili wa marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, aliyefariki dunia majuzi Hospitali ya Apollo nchini India, alipokuwa amelazwa akitibiwa. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo Jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment