Makamu Mwenyekiti Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.Hamid M. Hamid (wapili kushoto) akisoma matokeo ya wagombea nafasi ya Urais leo jijini Dar es Salaam katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu,anayemfuata kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva.
Baadhi ya waandishi wa Habari wa Ndani na Nje ya nchi wakifuatilia zoezi la kutangazwa kwa matokeo ya wagombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Msaidizi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema Bw. Matson Chizi akihojiwa na mwandishi wa habari wa Idhaa ya Kiswahili, Sauti ya Ujerumani (DW) Bi.Hawa Bihoga kuhusu namna gani analiona zoezi la utangazaji wa matokeo linafanyika.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva wanne kushoto kwa waliyokaa katika picha ya pamoja kwa baadhi na waangalizi wa uchaguzi kutoka nchi za Jumuiya ya SADC walipotembea ukumbi unaotumika kutangazia matokeo ya wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa habari kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Edward Kondela akimhoji mmoja wa waangalizi wa uchaguzi ambaye ni Mwenyekiti wa SADC nchini Malawi Bw.Justice Mbendera alipotembelea ukumbi wa kutangazia matokeo ya urais leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Anitha Jonas – MAELEZO.
No comments:
Post a Comment