Thursday, October 29, 2015

RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI

1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata  Mulamula (kulia ) akizungumza na Msaidizi wa Rais  wa masuala ya Kidplomasia, Zuhura Bundara (kushoto). Katikati  ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano  cha wizara hiyo, Mindi Kasiga.
2
Rais  wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Dkt  Jakaya Kikwete akiwa  katika picha ya pamoja  na Balozi wa Philippines nchini Bayani  Mangibin mara baada ya kuwasili   Ikulu   jijini Dares Salaam Oktoba 29, 2015 kwa ajili ya kukabidhi hati ya utambulisho  kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya  Kikwete.
unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Misri nchini Yasser Ahmed Elshawaf mara baada ya kuwasili   Ikulu   jijini Dares Salaam Oktoba 28, 2015 kwa ajili ya kukabidhi hati ya utambulisho . Kulia wa pili ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata  Mulamula.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wanne wanaziwakilisha nchi zao hapa Tanzania.Mabalozi waliowasilisha hati zao kwa Rais Kikwete ikulu Jijini Dar es Salaam Oktoba 28, 2015 ni pamoja Mhe.Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf Balozi mpya wa Misri hapa nchini, Mhe.Yahel Vilan Balozi mpya wa Israel nchini Tanzania, Mhe.Bayani Mangibin balozi mpya wa Ufilipino nchini na Mhe. Tan Puay Hiang Balozi mpya wa Singapore nchini Tanzania.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...