Thursday, May 29, 2014

SAFARI YA MWISHO YA MPENDWA MWANDISHI WA HABARI MAXIMILLIAN NGUBE HAPA DUNIANI

            
Baadhi ya ndugu na jamaa wakifarijiwa na wakazi wa jiji waliofika katika msiba huo wa Mpigapicha wa Kituo cha Televisheni cha Mlimani marehemu Maxmillian John Ngube.

Wakazi wa jiji waombolezaji wakiwa kati mstari wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu
                 Mke wa marehemu Suzy Jacob akiushika mwili wa  mumewe wakati  wa kuaga viwanja vya leaders Dar es Salaam.                            
Jeneza la mwili wa marehemu likishushwa katika kaburi.                                        Mchungaji (kushoto) akiendesha sala wakati wa maziko.                              Mmoja wa watoto wa marehemu akilia kwa uchungu wakati wa kuweka udongo katika kaburi la baba yake.           Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika huzuni kubwa wakati wa maziko hayo

Wabunge wa CUF kutoka Zanzibar Walipotaka kumtandik’ Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy. akikataa kupigwa picha wakati wakati huku wabunge wa cuf wakifuata nyuma na kumuoinyesha vidole kwa kutaka asimame ili wapambanekutokana na baada ya mbunge wa nkasi Ali kessy kutoa maneno ya kashfa kwa wabunge wa zanzibar wakati wa uchangiaji wa bajeti ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wakati wa maneno hayo pamoja na madai zanzibar ni nchi ndogo sawa na jimbo lake la nkasi

Tazama Picha Mbalimbali za Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa 27 Mei 2014

 Mwakilishi kutoka Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Betty Machangu (Mb.) akiwasilisha Hotuba kwa niaba ya Kamati hiyo
 Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje kutoka Kambi ya Upinzani, Mhe. Ezekiel Wenje nae akiwasilisha hotuba ya kambi yake.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwasilisha Bungeni  Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2014/2015 mjini Dodoma tarehe 27 Mei 2014
 
 Wanafunzi kutoka Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam wakifuatilia mijadala ya Bunge wakati wakijadili na kupitisha bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
 Katibu Mtendajii wa Jumuiya ya Maedneleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, Dkt. Stergomena Tax (katikati) akiwa na wageni wengine wakifutilia Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka 2014/2015
 Watendaji  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia hotuba.
  Baadhi ya Wawakilishi kutoka Balozi za nchi mbalimbali zilizopo hapa nchini wakifuatilia Hotuba ya Mhe. Membe (hayupo pichani)

Wednesday, May 28, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA ALIKUWA HANANG

1aKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu wakati alipopokelewa katika wilaya ya Hanang mpakani mwa mikoa ya Singida na Manyara akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwa uoande mwingine na wananchi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2010, Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa huyo anaongoza na Nape Nnauye katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM, Kinana amekumbana na kero kadhaa hasa suala zima la migogoro ya ardhi ambapo wananchi katika kijiji cha Gidika kata ya Gedabi huko Basotu wilayani Hanang. Wamemtaarifu katibu mkuu huyo  juu ya mgogoro wa ugawaji wa yaliyokuwa mashamba ya GAWAL yaliyokuwa yanamilikiwa na  NAFCO ambapo badala ya kugawiwa wanachi ambao ni wafugaji na wakulima viongozi wa kijiji hicho wamewauzia watu wachache ambao siyo wakazi wa kijiji hicho, jambo ambalo linawafanya wanakijiji hao kukosa haki ya kumiliki mashamba hayo. Hivyo kukosa  eneo la kilimo na ufugaji, Katibu mkuu huyo amewaagiza Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh. Erasto Mbwilo na mkuu wa wilaya ya Hanang kushughulikia suala hilo na kuhakikisha wananchi waliowengi wanapata haki yao badala ya kufaidika watu wachache.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE.HANANG- MANYARA)1aaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kiutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya ofisi za CCM wilaya ya Hanang mjini Katesh na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.1aaaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mh. Fredrick Sumaye  Waziri Mkuu mstaafu wakati alipowasili katika wilaya ya Hanang kuendelea na ziara yake mkoani Manyara.2Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mh. Fredrick Sumaye Waziri Mkuu Mstaafu wakati msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ulipowasili wilayani Hanang.2aKatibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi waliojitokeza kwa maelfu katika mkutano  wa hadhara uliofanyika mjini Katesh wilayani Hanang.3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Manyara wakati alipowasili wilayani Hanang.5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na mbunge wa jimbo la Hanang na Waziri wa Uwezeshaji  Mh. Dr. mary Nagu wakati alipowasili wilayani Hanang.6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye wakicheza ngoma ya asili ya watu wa Hanang wakati alipowasili katika kata ya Mwahu wilayani Hanang.7Wasichana wakicheza ngoma ya asili ya mkoa wa Manyara.8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wakati akipaua jengo la maabara katka shule ya sekondari ya Mwahu wilayani Hanang.9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye katika wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakishiriki katika ujenzi huo.12Kikundi cha ngoma kikiwa kinatumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Basotu.13Bw. Agustino Mayumba Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Hanang akiuiza swali kuhusu mnara wa simu uliojengwa katika katika eneo la soko kata ya Basotu wakati alipokuwa akihiji mapato ya kodi za mnara huo zinaenda wapi. hata hivyo iligundulika kwamba B, Agostino mayembe ndiye aliyesaini mkataba huo hivyo anajua mkataba uko wapi, Kushoto ni Napwe Nnauye.14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Bw. Agustino Mayumba Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Hanang wakati alipobananishwa na maswali kutoka kwa wananchi mbele ya Ndugu Abdulrahman Kinana huku akitakiwa kueleza juu ya mgogoro huo wa mapato ya mnara wa Simu wa Vodacom uliojengwa katika soko la Basotu.16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Amani Lucas Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya GENDABI Hanang wa pili kutoka kulia mara baada ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi, kulia ni Meshack Kimu  na Elisante Paulo Katibu wa tawi CHADEMA ambao wamejiengua  na kujiunga na CCM.21Warembo wakijiandaa kutoa burudani22Maelfu ya wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika kutano wa hadhara mjini Kates Hanang23Mh. Dr. Mary Nagu Mbunge wa jimbo la Hanang na Waziri wa uwezeshaji akizungumza na wananchi katika mkutano huo uliofanyika mjini Katesh;24Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kuvishwa kikoi vazi la heshima na kutawazwa mzee wa heshima  Katesh Hanang.25Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na Dr. Mary Nagu mbunge wa jimbo la Hanang wakikabidhi mizinga ya kufugia nyuki  ikiwa ni jitihada za mbunge wa jimbo la Hanang  kuvikwamua kiuchumi vikundo mbalimbali vya vijana. 1aaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Hanang.22Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika kutano huo.

Monday, May 26, 2014

AIRTEL YAFUNGUA DUKA LA KISASA MWANZA


Mratibu mwandamizi wa polisi  mkoa wa Mwanza SSP  Christopher Cyprian Fuime,  akikata utepe kuzindua duka la Airtel Mwanza mara baada ya matengenezo na kulifanya duka hilo kuwa la kisasa, pembeni yake ni Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba akiwa pamoja na wafanyakazi wa Airtel Mwanza. Uzinduzi huu umefanyika mwisho mwa wiki hii
Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba (kulia) akimwonyesha mgeni rasmi Mratibu mwandamizi wa polisi  mkoa wa Mwanza SSP  Christopher Cyprian Fuime kaunta maalumu zilizotengenezwa kwenye duka jipya kuhakikisha usalama katika huduma ya Airtel money wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel lililopo Mwanza, akishuhudia ni Violet Gyumi Afisa mauzowa Airtel kanda ya ziwa
Mratibu mwandamizi wa polisi  mkoa wa Mwanza SSP  Christopher Cyprian Fuime  akipewa maelezo na mfanyakazi wa kitengo cha wateja wakati wa uzinduzi wa dula la Airtel Mwanza, pichani ni Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba  pamoja na wafanyakazi wa Airtel
Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba (kushoto) akitoa maelezo kwa Mratibu mwandamizi wa polisi  mkoa wa Mwanza SSP  Christopher Cyprian Fuime kuhusu sehemu mbalimbali za duka jipya la mwanza wakati wa uzinduzi wa duka hilo ulifanyika mwishoni mwa wiki , pichani kulia ni Afisa mauzo wa Airtel kanda ya ziwa Violet Gyumi
Wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa duka la kisasa lililopo mwanza.
Afisa mauzo wa Airtel kanda ya ziwa Violet Gyumi akitoa zawadi kwa wateja waliohudhuria halfa ya ufunguzi wa duka la Airtel Mwanza uliofanyika mwishoni mwa wiki
Mrakibu mwandamizi wa polisi  mkoa wa Mwanza SSP  Christopher Cyprian Fuime,  ameipongeza Airtel kwa kuboresha mazingira ya maduka yao  kuwa ya kisalama zaidi kwa watumiaji wa huduma zao mbalimbali husasani ya Airtel Money.
SSP Christopher Cyprian Fuime,   aliyasema hayo kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola  wakati wa uzinduzi wa duka la kisasa la Airtel lilipo Mwanza uliofanyika mwishoni mwa wiki hii.
SSP Fuime alisema” nimefurahishwa sana na maboresho makubwa katika duka hili  ambayo yatawawezesha wakazi wa Mwanza na wateja wa Airtel kupata huduma bora kwa haraka zaidi katika mazingira mazuri.
Duka hili sasa linawahakikishia watej usalama zaidi  wanapofanya miamala ya fedha kupitia counter maalumu zilizowekwa kwaajili ya kuhakikisha usalama wa wateja na mali zao.
Sisi kama polisi tulionadhamana ya kuhakikisha usalama wa raia tunawapongeza sana Airtel kwa kuliona hili na kuhakikisha huduma ya Airtel Money inatolewa katika mazingira yaliyo na usalama”.
“Tunawashauri wateja na wakazi wa Mwanza kupata muda na kutembelea duka hili na kufurahia huduma zinazotelewa hapa”. Aliongeza SSP Fuima
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba alisema” Tunaendelea na mradi wetu wa kuboresha maduka yetu na kuyafanya yawe ya kisasa zaidi , leo tunazindua duka letu la mwanza baada ya matengenezo,
mwonekano huu mpya ulioboreshwa zaidi utatuwezesha kutoa huduma kwa ufanisi , haraka zaidi kupitia kaunta zilizowekwa kwaajili ya kuhudumia wateja. sasa wateja watahudumia kwa haraka bila kupoteza muda.
Sambamba na hilo tumeboresha sehemu za kutoa na kutuma pesa kwa kuweka kaunta maalumu zilizo za kisalama zaidi zitakazowawezesha wateja wetu kutumia huduma ya Airtel Money kwa usalama zaidi.

Huu ni mwanzo tu katika kuhakikiksha tunato huduma bora na kuwapatia wateja wetu uzoefu tofauti katika huduma zetu. Mpango ni kufungua matawi zaidi na kuboresha maduka yetu yote nchi ili yawe ya kisasa kama hili la mwanza, Arusha na Mlimani City Dar ambayo tayari tumeshayazindua aliongeza Lyamba.

Marais Waondoka Baada ya Kushuhudia Kuapishwa Kwa Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma

 Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiondoka Union Buildings baada ya kushuhudia Rais Jacob Zuma akiapa kuwa Rais wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika jingo la Union Buildings mjini Pretoria, Afrika Kusini,  Mei 24, 2014
 Marais na viongozi toka nchi mbalimbali wakiondoka Union Buildings baada ya kushuhudia Rais Jacob Zuma akiapa kuwa Rais wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika jingo la Union Buildings mjini Pretoria, Afrika Kusini,  Mei 24, 2014.
 Ndege za kijeshi zikiunda umbo la "20" kuashiria miaka ishirini ya uhuru kamili wa Afrika Kusini  katika sherehe za kuapa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika jingo la Union Buildings mjini Pretoria, Afrika Kusini,  Mei 24, 2014.Picha na IKULU

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...