Friday, May 16, 2014

PROIN PROMOTIONS YATANGAZA RASMI KUDHAMINI LIGI YA MPIRA WA MIGUU KWA WANAWAKE JIJINI DAR ES SALAAM

Katibu wa Michezo kutoka Kampuni ya Proin, Godlisten Anderson akitambulisha viongozi wa kampuni ya Proin Promotions kwa waandishi wa habari wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Southern Sun. Kampuni ya Proin imetangaza kudhamini ligi ya mpira wa miguu kwa Wanawake inayotarajiwa kuanza Mwezi wa Nane.
Rais TFF, Mh Jamal Malinzi na Mwenyekiti wa makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza wakitia saini katika mkataba wa makubaliano ya udhamini wa ligi ya mpira wa miguu kwa wanawake itakayoanza mwezi wa Nane.
Raisi wa TFF, Mh Jamal Malinzi (kushoto) akibadilishana mkataba wa udhamini na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza (katikati) mara baada ya kumaliza kutiliana saini katika mikataba hiyo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Southern Sun.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Cha Wanawake, Bi Lina Muhando akiongea na Waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Sourthen Sun wakati Kampuni ya Proin ilitangaza kudhamini ligi ya wanawake inayotarajiwa kuanza Mwezi wa Nane.
Rais Wa TFF, Mh Jamal Malinzi akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kuweka saini katika Mkataba wa Udhamini kati ya Proin Promotions na TFF
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza akijibu maswali ya waandishi wa habari katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hotel ya Southern Sun.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...