Monday, May 26, 2014

AIRTEL YAFUNGUA DUKA LA KISASA MWANZA


Mratibu mwandamizi wa polisi  mkoa wa Mwanza SSP  Christopher Cyprian Fuime,  akikata utepe kuzindua duka la Airtel Mwanza mara baada ya matengenezo na kulifanya duka hilo kuwa la kisasa, pembeni yake ni Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba akiwa pamoja na wafanyakazi wa Airtel Mwanza. Uzinduzi huu umefanyika mwisho mwa wiki hii
Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba (kulia) akimwonyesha mgeni rasmi Mratibu mwandamizi wa polisi  mkoa wa Mwanza SSP  Christopher Cyprian Fuime kaunta maalumu zilizotengenezwa kwenye duka jipya kuhakikisha usalama katika huduma ya Airtel money wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel lililopo Mwanza, akishuhudia ni Violet Gyumi Afisa mauzowa Airtel kanda ya ziwa
Mratibu mwandamizi wa polisi  mkoa wa Mwanza SSP  Christopher Cyprian Fuime  akipewa maelezo na mfanyakazi wa kitengo cha wateja wakati wa uzinduzi wa dula la Airtel Mwanza, pichani ni Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba  pamoja na wafanyakazi wa Airtel
Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba (kushoto) akitoa maelezo kwa Mratibu mwandamizi wa polisi  mkoa wa Mwanza SSP  Christopher Cyprian Fuime kuhusu sehemu mbalimbali za duka jipya la mwanza wakati wa uzinduzi wa duka hilo ulifanyika mwishoni mwa wiki , pichani kulia ni Afisa mauzo wa Airtel kanda ya ziwa Violet Gyumi
Wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa duka la kisasa lililopo mwanza.
Afisa mauzo wa Airtel kanda ya ziwa Violet Gyumi akitoa zawadi kwa wateja waliohudhuria halfa ya ufunguzi wa duka la Airtel Mwanza uliofanyika mwishoni mwa wiki
Mrakibu mwandamizi wa polisi  mkoa wa Mwanza SSP  Christopher Cyprian Fuime,  ameipongeza Airtel kwa kuboresha mazingira ya maduka yao  kuwa ya kisalama zaidi kwa watumiaji wa huduma zao mbalimbali husasani ya Airtel Money.
SSP Christopher Cyprian Fuime,   aliyasema hayo kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola  wakati wa uzinduzi wa duka la kisasa la Airtel lilipo Mwanza uliofanyika mwishoni mwa wiki hii.
SSP Fuime alisema” nimefurahishwa sana na maboresho makubwa katika duka hili  ambayo yatawawezesha wakazi wa Mwanza na wateja wa Airtel kupata huduma bora kwa haraka zaidi katika mazingira mazuri.
Duka hili sasa linawahakikishia watej usalama zaidi  wanapofanya miamala ya fedha kupitia counter maalumu zilizowekwa kwaajili ya kuhakikisha usalama wa wateja na mali zao.
Sisi kama polisi tulionadhamana ya kuhakikisha usalama wa raia tunawapongeza sana Airtel kwa kuliona hili na kuhakikisha huduma ya Airtel Money inatolewa katika mazingira yaliyo na usalama”.
“Tunawashauri wateja na wakazi wa Mwanza kupata muda na kutembelea duka hili na kufurahia huduma zinazotelewa hapa”. Aliongeza SSP Fuima
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba alisema” Tunaendelea na mradi wetu wa kuboresha maduka yetu na kuyafanya yawe ya kisasa zaidi , leo tunazindua duka letu la mwanza baada ya matengenezo,
mwonekano huu mpya ulioboreshwa zaidi utatuwezesha kutoa huduma kwa ufanisi , haraka zaidi kupitia kaunta zilizowekwa kwaajili ya kuhudumia wateja. sasa wateja watahudumia kwa haraka bila kupoteza muda.
Sambamba na hilo tumeboresha sehemu za kutoa na kutuma pesa kwa kuweka kaunta maalumu zilizo za kisalama zaidi zitakazowawezesha wateja wetu kutumia huduma ya Airtel Money kwa usalama zaidi.

Huu ni mwanzo tu katika kuhakikiksha tunato huduma bora na kuwapatia wateja wetu uzoefu tofauti katika huduma zetu. Mpango ni kufungua matawi zaidi na kuboresha maduka yetu yote nchi ili yawe ya kisasa kama hili la mwanza, Arusha na Mlimani City Dar ambayo tayari tumeshayazindua aliongeza Lyamba.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...