Wednesday, May 28, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA ALIKUWA HANANG

1aKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu wakati alipopokelewa katika wilaya ya Hanang mpakani mwa mikoa ya Singida na Manyara akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwa uoande mwingine na wananchi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2010, Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa huyo anaongoza na Nape Nnauye katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM, Kinana amekumbana na kero kadhaa hasa suala zima la migogoro ya ardhi ambapo wananchi katika kijiji cha Gidika kata ya Gedabi huko Basotu wilayani Hanang. Wamemtaarifu katibu mkuu huyo  juu ya mgogoro wa ugawaji wa yaliyokuwa mashamba ya GAWAL yaliyokuwa yanamilikiwa na  NAFCO ambapo badala ya kugawiwa wanachi ambao ni wafugaji na wakulima viongozi wa kijiji hicho wamewauzia watu wachache ambao siyo wakazi wa kijiji hicho, jambo ambalo linawafanya wanakijiji hao kukosa haki ya kumiliki mashamba hayo. Hivyo kukosa  eneo la kilimo na ufugaji, Katibu mkuu huyo amewaagiza Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh. Erasto Mbwilo na mkuu wa wilaya ya Hanang kushughulikia suala hilo na kuhakikisha wananchi waliowengi wanapata haki yao badala ya kufaidika watu wachache.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE.HANANG- MANYARA)1aaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kiutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya ofisi za CCM wilaya ya Hanang mjini Katesh na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.1aaaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mh. Fredrick Sumaye  Waziri Mkuu mstaafu wakati alipowasili katika wilaya ya Hanang kuendelea na ziara yake mkoani Manyara.2Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mh. Fredrick Sumaye Waziri Mkuu Mstaafu wakati msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ulipowasili wilayani Hanang.2aKatibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi waliojitokeza kwa maelfu katika mkutano  wa hadhara uliofanyika mjini Katesh wilayani Hanang.3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Manyara wakati alipowasili wilayani Hanang.5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na mbunge wa jimbo la Hanang na Waziri wa Uwezeshaji  Mh. Dr. mary Nagu wakati alipowasili wilayani Hanang.6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye wakicheza ngoma ya asili ya watu wa Hanang wakati alipowasili katika kata ya Mwahu wilayani Hanang.7Wasichana wakicheza ngoma ya asili ya mkoa wa Manyara.8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wakati akipaua jengo la maabara katka shule ya sekondari ya Mwahu wilayani Hanang.9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye katika wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakishiriki katika ujenzi huo.12Kikundi cha ngoma kikiwa kinatumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Basotu.13Bw. Agustino Mayumba Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Hanang akiuiza swali kuhusu mnara wa simu uliojengwa katika katika eneo la soko kata ya Basotu wakati alipokuwa akihiji mapato ya kodi za mnara huo zinaenda wapi. hata hivyo iligundulika kwamba B, Agostino mayembe ndiye aliyesaini mkataba huo hivyo anajua mkataba uko wapi, Kushoto ni Napwe Nnauye.14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Bw. Agustino Mayumba Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Hanang wakati alipobananishwa na maswali kutoka kwa wananchi mbele ya Ndugu Abdulrahman Kinana huku akitakiwa kueleza juu ya mgogoro huo wa mapato ya mnara wa Simu wa Vodacom uliojengwa katika soko la Basotu.16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Amani Lucas Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya GENDABI Hanang wa pili kutoka kulia mara baada ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi, kulia ni Meshack Kimu  na Elisante Paulo Katibu wa tawi CHADEMA ambao wamejiengua  na kujiunga na CCM.21Warembo wakijiandaa kutoa burudani22Maelfu ya wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika kutano wa hadhara mjini Kates Hanang23Mh. Dr. Mary Nagu Mbunge wa jimbo la Hanang na Waziri wa uwezeshaji akizungumza na wananchi katika mkutano huo uliofanyika mjini Katesh;24Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kuvishwa kikoi vazi la heshima na kutawazwa mzee wa heshima  Katesh Hanang.25Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na Dr. Mary Nagu mbunge wa jimbo la Hanang wakikabidhi mizinga ya kufugia nyuki  ikiwa ni jitihada za mbunge wa jimbo la Hanang  kuvikwamua kiuchumi vikundo mbalimbali vya vijana. 1aaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Hanang.22Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika kutano huo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...