Tuesday, May 13, 2014

WANANCHI WA JIMBO LA IGALULA WAMNING’NIZA MFUTAKAMBA MBELE YA KINANA

Kauli hiyo ya Ndugu Abdulrahman Kinana imekuja baada ya wananchi kuonyesha waziwazi kutokubali utendaji kazi wa mbunge huyo ambaye aliwekwa kitimoto na wananchi hao, wakisema amekuwa akipiga porojo tu badala ya kutatua matatizo yanayowakabili  huku wakitolea mfano wa zahahati ya kata hiyo ambayo haina Jokofu la kuhifadhia dawa kwa zaidi ya miaka mitano sasa, jambo ambalo linawafanya akina mama wajawazito pamoja na wagonjwa wengine kupata adha kubwa kutokana na kukosa dawa katika zahanati hiyo, Wananchi hao wameongeza kuwa mara baada ya kuchaguliwa  mbunge huyo aliwaahidi kuleta mnara wa mawasiliano wa simu za mkononi kwa muda wa siku 100 jambo ambalo halijatekelezwa mpaka sasa.Hata hivyo Katibu Mkuu Kinana ameahidi kuwanunulia jokofu hilo wananchi wa kata ya Loya ili kuondokana na adha hiyo (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UYUI-TABORA)3aKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea kuwahutubia wananchi.
4aNape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kizendi wilayani Uyui .5Moja ya nyumba za walimu zilizojengwa katika shule ya sekondari ya Lutende wilayani Uyui.5aMwenyekiti wa CCM Wilaya ya Uyui Ndugu Mussa Ntimizi akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrhman Kinana ili kuzungumza na wananchi.6Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akipanda mti wa kumbukumbu katika shule sekondari ya Lutende.6aNape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akisisitiza jambo wakati akihuwahutubia wananchi hao.7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  wa pili kutoka kulia akikagua nyumba ya walimu katika shule ya sekondari ya Lutend kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi  na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Fatma Mwassa.8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua shina la wakereketwa katika kijiji cha Miyenze kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM kijiji cha Miyenze Bw. Jawali Masinde.9Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Fatma Mwassa akijibu hoja ya moja wa wananchi aliyekuwa akihoji juu ya suala la kupatiwa maeneo ya kucchungia mifugo yao kutoka hifadhi ya inayopakana na kijiji hicho mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati ni Mbunge wa jimbo la Igalula Mh. Athman Mfutakamba na Nape Nnauye mwenye kofia10Hii ni msafiri kafiri11Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagumaktaba ya shule ya sekondari ya Loya12Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua moja ya madarasa yaliyojengwa katika shule hiyo anayefuatana naye ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui Ndugu Mussa Ntimizi.13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ofisi ya CCM kata ya Loya kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui Ndugu Mussa Ntimizi.14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na vijana timu za mpira za kata hiyo kulia ni Mbunge wa jimbo la Igalula Athman Mfutakamba na katikati ni Mussa Ntimizi mwenyekiti wa CCM Uyui.15Vijana wa Sungusungu wakicheza ngoma.16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vijana wa sungusungu pamoja na wazeee wa kata ya Kizengi.17Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.18Wananchi wakiwa katika mkutano huo19Hawa sio askari wa usalama barabarani ni vijana wakicheza moja ya ngoma zinazochezwa na wenyeji wa mkoa wa Tabora.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...