Thursday, July 11, 2013

Ujumbe wa Rais wa Sierra Leone watembelea Shirika la Nyumba la Taifa




 Meya wa Jiji la Freetown, Sierra Leone, Mheshimiwa Sam Franklyn Bababode Gibson (kulia) na ujumbe wake akifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa kwenye chumba cha mikutano.
 Ujumbe wa Sierra Leone ukiwa njiani kuelekea kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Kibada


Ujumbe wa Serikali ya Sierra Leone kutoka jiji la Freetown ulipotembelea ukiongozwa na Meya wa Jiji Mheshimiwa Sam Franklyn Bababode Gibson uliotembelea Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na miradi yake ya ujenzi.

Ujumbe wa Serikali ya Sierra Leone umetembelea Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuweza pamoja na mambo mengine kujifunza namna Shirika hilo linavyofanya kazi zake na namna lilivyoweza kufanikiwa.
Akizungumza na watendaji mbalimbali wa NHC alipofika makao makuu ya shirika hilo, Meya wa Jiji la Free Town, Sierra Leone, Mheshimiwa Sam Franklyn Bababode Gibson aliwasilisha salamu za Rais Ernest Bai Koroma akisema kwamba Rais huyo amevutiwa namna Shirika linavyofanya kazi na ndiyo maana wamekuja kujifunza.
Alifurahishwa na mipango ya Shirika la Nyumba ya kujenga nyumba bora zinazowezesha watu kuishi vizuri
“Tumetembelea eneo la Kibera Kenya na kuona namna maisha ya binadamu yalivyo katika tishio na akaisifu Tanzania hususan Shirika la nyumba kwa kuwa na makazi yaliyopangwa  na namna linavyotenda kazi na hivyo watajaribu kufuata nyayo za Shirika hilo,”alisema.
Alisema alichokiona katika kitongoji hicho ni mbaya ikiwa imegubikwa na umaskini wa kutisha na wakazi wakikosa huduma muhimu kama umeme na maji safi.
Kibera ndiyo eneo kubwa la watu wa kipato cha chini na ndilo eneo linaloshikilia rekodi ya kuwa eneo la pili kwa makazi holela barani Afrika.
Kwa mujibu wa takwimu ya sensa na makazi iliyofanyika mwaka 2009, idadi ya wakazi wa Kibera ni 170,070, tofauti na ilivyokuwa inakadiriwa kwamba idadi ya wakazi ni kati ya milioni moja au 2.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Susan Omari alisema kuwa ziara hiyo ni muhimu sana kwa Shirika kwani pamoja na wageni hao kuja kujifunza Tanzania, Shirika pia limejifunza mengi na ambayo yatasaidia katika  kuboresha mipango mbalimbali ya Shirika.
Walikuwa katika ziara ya kuytembelea miji wakianzia Kenya, walitembelea makao makuu ya NHC Tanzania na kufurahishwa na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambao utasaidia wananchi wengi na hivyo kuondoa tatizo la makazi pia walifurahishwa na teknolojia ya hydraform inayotumika kufyatulia matofali kwani inatumia sementi kidogo na hivyo kupunguza gharama.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...