Monday, July 15, 2013

BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI MAREKANI LIBERATA MULAMULA AWASILI WASHINGTON, DC


Balozi Liberata Mulamula akishuka kwenye gari Bethesda, Maryland wakati akitokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia Ijumaa July 12, 2013. Mhe, Mulamula ndiye Balozi wa Tanzania nchini Marekani aliyekuja kuchukua nafasi ya Balozi Mwanaidi Maajar aliyemaliza muda wake mwanzoni mwa mwaka huu. Kabla ya hapo Balozi Mulamula alikua Balozi wa maziwa makuu na msaidizi wa Rais mwandamizi katika maswala ya diplomasia.

Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliofika kumlaki kwenye yatakayokua makazi yake Bethesda, Maryland.

 Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliofika kumlaki kwenye yatakayokua makazi yake Bethesda, Maryland.
Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi (hawapo pichani) wakati walipomkaribisha nyumbani kwake, Bethesda, Maryland.
Watoto wa Mhe. Balozi Alvin na Tanya.
 Mume wa Mhe. Balozi, Bwn. George Mulamula.
Kaimu Balozi na mkuu wa Utawala na Fedha, Mama Lily Munanka katika picha.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akibadlishana mawili matatu na Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakati walipomkaribisha nyumbani kwake Bethesda, Maryland kushoto ni Afisa Ubalozi Mindi Kasiga.

 Juu na chini ni Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakiwa tayari kumpokea Mhe. Balozi Mulamula na familia yake.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...