Wafuasi wa Chadema wakiandamana kuelekea katika ofisi za Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kwenda kumpongeza kwa kusimamia vizuri uchaguzi wa Madiwani.
Wafuasi wa CHADEMA wakishangilia ushindi katika maandamano ya amani ya madiwani wapya na viongozi kwenda kumpongeza Mkurugenzi wa jiji kwa kusimamia uchaguzi vizuri.
Lema akiwa na madiwani wapya wakiingia katika jingo la Halmashauri kuonana na Mkurugenzi wa jiji
Madiwani wapya waliochaguliwa jana na wabunge wa CHADEMA wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa jiji la Arusha Sipora Liana jana walipofika ofisini kwake kumpongeza kwa kusimamia vizuri uchaguzi madiwani.
OCD wa Arusha Gilles Mulloto akimisihi Mbunge wa Arusha awatawanye wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamekusanyika nje ya jingo la Halmashauri wakiwasubiri viongozi wao waliokuwa wamekwenda kuonana na Mkurugenzi wa jiji kumpongeza kwa kusimamia vizuri uchaguzi wa jana,wafuasi hao na viongozi hao walifanya maandamano ya amani jana.
No comments:
Post a Comment