Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Fabia Massawe baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba leo tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku sita mkoani humo
Rais Kikwete akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman ambaye pia yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi
Rais Kikwete akisalimiana na Mstahiki Meya wa Bukoba Mhe Anatory Amani
Vijana wa Skauti wa Bukoba wakimlaki Rais Kikwete uwanjani hapo
Wanahabari toka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kazini
Kijana wa Skauti akipiga saluti kuomba kumvisha skafu Rais Kikwete
Rais Kikwete akivishwa skafu
Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli. Kushoto ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe
Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
Rais Kikwete akisalimiana na viongozi na wananchi waliofika uwanjani kumlaki
Rais Kikwete akisalimiana na Mkuu wa JKT
Rais Kikwete akisalimiana na viongozi wa dini mbalimbali waliokuwepo uwanjani
Rais Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni
Ngoma ya Kihaya ikimlaki Rais Kikwete Bukoba
Karibu Bukoba mheshimiwa Rais....
Sehemu ya viongozi waliohudhuria sherehe ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba
Viongozi wa dini wakiwa bega kwa bega kwenye sherehe hizo
Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akimkaribisha Rais Kikwete kuongea na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba
Rais Kikwete akiongea na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
Rais Kikwete akipata maelezo kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
Rais Kikwete akifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe Peter Serukamba wakishangilia wakati Rais Kikwete akiweka jiwe la msingi
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wadau baada ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
Rais Kikwete akisalimiana na Mhashamu Methodius Kilaini, Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba
Sehemu ya uwanja wa ndege wa Bukoba unaokarabatiwa na kupanuliwa
Rais Kikwete akiwasili Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Rais Kikwete akisalimiana na wanachama wa KCU alipowasili Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Rais Kikwete akisalimiana na wananchi waliofurika kushuhudia ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Rais Kikwete akiendelea kusalimia wananchi
Mwenyekiti wa Bodi ya KCU (1990)LTD John Binushu akimkaribisha Rais Kikwete Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Sehemu ya umati wa wananchi kwenye ufunguzi wa jengo hilo
Jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Rais Kikwete akipokea risala toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya KCU (1990)LTD John Binushu
Rais Kikwete akipokea zawadi ya kahawa toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya KCU (1990)LTD John Binushu
Rais Kikwete akifunua kitambaa kama ishara ya Kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Rais Kikwete akikata utepe Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Rais Kikwete akihutubia wananchi baada ya Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Wananchi wakimsikiliza Rais Kikwete
Rais Kikwete akihutubia
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa KCU baada ya kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
--
Ndugu Wananchi, kama ambavyo nimewahi kuwajulisha mara nyingi kupitia vyombo vyetu vya habari juu ya Mkoa wetu wa Kagera kupewa heshima kubwa ya kuandaa maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kitaifa mwaka 2013, leo napenda kuwajulisha juu ya maandalizi ya maadhimisho hayo ambayo yataadhimishwa tarehe 25/07/2013 hapa mkoani kwetu katika Wilaya ya Muleba katika Kambi ya Jeshi la Wananchi Kaboya. Pia nawajulisha kuwa maadhimisho hayo yataambatana na ziara ya kikazi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkoa wa Kagera.
MAADHIMISHO YA MASHUJAA MWAKA 2013
Ndugu Wananchi, Maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Kumbumbu ya Mashujaa mkoani Kagera yanaendelea vizuri kamati mbalimbali za maandalizi zinatekeleza majukumu yake ya mwisho ili kufanikisha maadhimisho siku ya Alhamisi ya wiki hii tarehe 25 Julai, 2013. Kamati zinazoandaa maadhimisho hayo ni Kamati ya Mapokezi, Usafiri na Malazi; Kamati ya Ujenzi Uwanja na Mapambo; Kamati ya Chakula na Afya; Kamati ya Ulinzi na Usalama; na Kamati ya Burudani, Habari na Uhamasishaji.
Ndugu wananchi, Kwa kiwango kikubwa maandalizi yote yamekamilika na tunatarajia kuanzia leo kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya mkoa, pia nje ya nchi watakaohudhuria maadhimisho hayo.
Mkoa wetu umejipanga vizuri kuwapokea wageni wote watakofika mkoani hapa kwa ukarimu na bashasha kubwa.
Wajibu wa Wananchi
Ndugu wananchi, Napenda kutumia fursa hii kuwaomba kuwa wakarimu kwa wageni wetu wote tunaowatarajia kuanzia leo kwa kutekeleza majukumu yenu kama Wanakagera kama ifuatavyo;
Ø Kila mwananchi kuhakikisha maeneo yake na mazingira yanayomzunguka yanaendelea kuwa katika hali ya usafi kama utamaduni wetu. Pia kumwajibisha mtu yeyote atakaeonekana anachafua mazingira yetu. Hili ni jukumu la kila mwananchi.
Ø Kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika kuadhimisha Siku yenyewe ya Kumbukumbu ya Mashujaa tarehe 25 Julai, 2013 huko Kaboya Wilayani Muleba. Kwani hatuna budi kuwakumbuka Mashujaa wetu kwa sababu ya historia ya mkoa wetu kushiriki katika vita ya kumwondoa adui aliyekuwa amevamia nchi yetu kupitia ardhi ya mkoa huu mwaka 1978 hadi 1979.
Ø Kila mwananchi kuhakikisha anaitunza amani na utulivu kama destuli ya mkoa wetu kwa wakati wote wageni wetu watakapokuwepo hapa mkoani na baada ya maadhimisho ya Mashujaa. Aidha, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imejipanga vizuri kuhakikisha amani na utulivu vinatawala wakati wote. Kwa mwananchi yeyote atakayeona viashiria vya uvunjifu wa amani atoe taarifa mara moja ili taarifa hizo zifanyiwe kazi mara moja.
Wajibu wa Vyombo vya Habari
Ndugu Wananchi, Vyombo vyetu vya habari vina wajibu wa kuhakikisha vinaendelea kutoa taarifa mbalimbali kwa wananchi kuhusu Maadhimisho ya Mashujaa kama ambavyo vimekuwa vikifanya kuanzia mwezi Mei, 2013.
Aidha, nawaombeni Waandishi, Wahariri na Wamiliki wa vyombo vya habari kutumia fursa hii kuutangaza mkoa wetu wa Kagera katika sekta mbalimbali za uwekezaji na fursa mbalimbali zinazopatikana katika mkoa wetu.
Vilevile nawaombeni Wamiliki wa vyombo vya habari hasa redio zetu za jamii kutoa muda wa kutosha katika vituo vyenu vya redio kurusha habari na matukio ya Kumbukumbu za Mashujaa papo kwa papo (live coverage) siku ya maadhimisho ili wananchi ambao hawatapata muda wa kufika Kaboya wazipate habari hizo kupitia redio zetu za Jamii.
ZIARA YA MHE. RAIS MKOANI KAGERA
Ndugu Wananchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye atakayekuwa mgeni Rasmi Katika Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa tarehe 25 Julai, 2013. Pia Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika mkoa wetu wa Kagera.
Ndugu Wananchi, Katika ziara hiyo Mheshimiwa Rais Kikwete anatarajia kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wetu kama ifuatavyo:
§ Kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
§ Kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Kagoma - Rusahunga
§ Kuweka jiwe la msingi barabara ya kiwango cha lami Kyaka hadi Bugene
§ Kufungua Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba.
§ Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
§ Kuzindua mradi wa maji Muleba
§ Kuzindua kivuko kipya Rusumo (Ngara)
§ Kuzindua mradi wa usambazaji umeme vijijini Nyaishozi (Karagwe)
§ Kuzindua Wilaya Mpya ya Kyerwa
Ndugu Wananchi, Vilevile Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataongea na wananchi kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara katika Wilaya zetu ndani ya mkoa.
Ndugu Wananchi, nawaombeni kujitokeza kuanzia tarehe 24/07/2013 uwanja wa ndege wa Bukoba ili kumpokea Mheshimiwa Rais, pia atakapokuwa anafanya ziara katika Wilaya zetu tujitokeze kwa wingi kumsikiliza.
Mwisho; Nawatakia ushiriki mzuri katika kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa na mapokezi mazuri ya wageni wetu hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kagera: Amani na Maendeleo.
Amani na Maendeleo; Kagera.
Imetolewa na: Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe
Mkuu wa Mkoa
KAGERA
No comments:
Post a Comment