Mwanamke anayedaiwa kupanga njama za kumuua mumewe wa ndoa na mtoto wa mume huyo, amepandishwa mahakamani akiwa na mtuhumiwa mwingine wa mauaji hayo.
Janeth Jackson (32), mkazi wa Moshono, Arusha na Novatus Elias, walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha /Arumeru, Devotha Kamuzora, wakisomewa makosa mawili ya kula njama ya kutaka kumuua Simon Jackson ambaye ndiye mume wa Janeth.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Edna Kasala, alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa wote walitenda kosa la pili la kula njama na kutaka kumuua Desderi Sabas, ambaye ni mtoto wa mke mwingine kwa mume huyo anayeishi Bukoba, mkoani Kagera.
Washtakiwa wote hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu Mahakama hiyo kisheria haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.Kasala iliomba mahakama kuwanyima dhamana washtakiwa, kwa sababu watuhumiwa wengine wawili wanatafutwa hivyo na upelelezi haujakamilika.Kwa Habari zaidi bofya na Endelea......>>>>>>
No comments:
Post a Comment